Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Mkuu huyu FaizaFoxy ni mdini balaa! Yaani kamwona Pengo tu; Mufti kwake sio issue. Sometimes huyu ni wa kupuuza tu.
Hivi tafsiri ya udini ni nini uwa napata tabu kufahamu ebu tufahamishe.
 
Last edited by a moderator:


Punguza udini utaeleweka. Lissu hajachambua mambo kidini bali kisiasa na ameeleweka vizuri sana. Sasa wewe na makuwadi wenzio mnapoanza kutuletea habari za Kariakoo na misikitini hamueleweki. Mnafiki mkubwa wewe.
 
Tusubiri, ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Kumbuka juzi, Sitta ingawa yupo busy bungeni lakini kaitwa na Pengo na kaenda mbio-mbio, jiuliize kunani?

Na wewe muongo, mzandiki mfitini na mnafiki mkubwa, Sitta aliomba kuonana na viongozi wa dini Pengo na Mufti Simba
 
Hivi tafsiri ya udini ni nini uwa napata tabu kufahamu ebu tufahamishe.

Mfuatilie FaizaFoxy na Mohamed Said role models wako utajua maana yake. Ukishafuzu kwa hao, nenda kwa Ponda upate daraja ya juu zaidi.
 
Punguza udini utaeleweka. Lissu hajachambua mambo kidini bali kisiasa na ameeleweka vizuri sana. Sasa wewe na makuwadi wenzio mnapoanza kutuletea habari za Kariakoo na misikitini hamueleweki. Mnafiki mkubwa wewe.
Wewe punguani kweli tafsiri yako ya udini mtu akiwa Muislam mambo ya Msikiti yameingiaje hapa kama siyo unafiki, kwako uwa hakuna Mkirsto mdini wadini wote ni Waislam.
 
Mimi nafurahi napoona malumbano ya namna hii na kujenga hoja kwenu,alicho kifanya lisu ni kuonyesha matendo yaliyofanywa kipindi hicho ambayo kimsingi yanaweza kuwa sahihi lakini kwa kipindi hiki yakawa ni mapungufu makubwa sana ambayo hayakuzingatia haki na uhuru wa kutoa maoni.

Sikubaliani na Muungano huu ambao kimsingi hata wazazi wetu hawaujui.
 
Hata Nyerere alishakiri kuna mambo ya kijinga serikali yake iliyafanya na akasema tuache ya kijinga tuchukue mazuri!
Kwa mtazamo wako, makosa ya Muungano kama Mh. Tundu Lissu alivyoyaanisha unayaweka wapi?.

Katika lundi la maamuzi ya kijinga au kiakili?.

Kama niya kijinga, mbona sasa wabunge wamejikita kwenye 'madudu' ya Muungano.

Kama niya kiakili, mbona wabunge wanahoji utaratibu uliotumika na nyaraka za kisheria.
 

Mze MUHAMED SAID Kamuelezea vizuri sana JKN lakini watu wanamuona Mze MS kama ana mchukia KJN kwa ukiristo wake.Lakini sasa nadhani waTz watamuamini MZE MS na wataamini kama Jkn mengi ktk utawala wake aliyakosea.
 
Nyerere mwenyewe alishasema alifanya mambo mazuri na ya kijinga pia! Kama hujui kaa kimya mdomo kunuka wewe
Je, aliwahi kuwaomba msamaha Watanzania kwa mambo ya kijinga aliyokiri kuwafanyia?
 
 
Wewe sasa ushahamia kwenye udini, sisi huko hatupo tunajadili muungano sie.

Kuna siku utanielewa.

Hata hili la uongo wa Nyerere nikishambuliwa sana humu, sasa limetokea kwa Lissu.
 
Mimi huwa sina hoja zenye mashiko bali huwa nina hoja za majadiliano katika kufikia makubaliano au kukubali kutokubaliana.

Mimi sitaki hata kusikia mtu ananiambia ananipenda. Ninachotaka ni kuheshimiwa kama nilivyoyaheshimu mawazo yako ingawa hayafai hata katika jamii pevu.

viroba ndiyo nini?.

Mdomo wangu kuwa mweusi unahusiana na nini katika kuandika. Kwani wewe unaandika kwa kutumia mdomo?.
 
Hawa wanasiasa waachane na Mwalimu Nyerere,kama katiba mpya imewashinda si wauvunje huu muungano,kila kitu Nyerere!ina maana Nyerere ndo pekee aliupenda muungano?waache siasa za kinafiki,hakuna mtakatifu kuliko Nyerere.
 

Kwa kadri ya evidence aliyotoa Tundu wakati anatoa hoja ya wachache kwamba hati ya Muungano haijapata kuwasilishwa UN wala haipo Tanzania baada ya Zanzibar kushindwa kuwasilisha hati hiyo mahakamani baada ya kesi (ya mwaka 2005) iliyoikabili dola hiyo kuhusu uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni dhahiri kuna walakin katika utawala wa Nyerere.

Huenda ni kutokana dosari hizo za kisheria iliyosababishwa na Nyerere na Karume zilimlazimisha Nyerere kumkabili yeyote yule aliyejaribu kuhoji Muungano kwa kile kinachojulikana kama kuhoji Muungano ni uhaini. Kama Muungano ulikuwa halali ni kwa nini Nyerere aliweka mwiko wa kutouhoji? Nyerere alijua fika Muungano hauna uhalali wowote ndiyo maana aliamua kuulinda kwa mkono wa chuma ili mwl asijeadhirika ikijulikana kwamba nchi hizo mbili ziliunganishwa kihuni.

Mimi nadhani hoja alizotoa Lisu zina mashiko. Kwa nini tuishi Muungano ambao hauna baraka za Watanganyika na Wazanzibar? Kwa nini Muungano ukose legal backup huku watawala wakishinikiza kuwa Muungano ni halali? Hati ya Muungano kuwa siri nzito maana yake nini? Kwa nini Muungano uruhusu nchi moja kubaki na identity yake huku nyingine ikifutwa juu ya uso wa dunia? Kwa nini inashindikana kuwa na Muungano wa nchi moja yenye serikali moja kama kweli watawala wanaamini udugu wanaouhubiri kati ya watanganyika na wazanzibari?

Kama kweli wazanzibari na watangayika ni ndugu wa damu kama inavyodaiwa na watawala wa sasa basi tuwe na serikali moja tu ya Muungano wa Tanzania; Zanzibar ifutike katika ramani ya dunia kama ilivyofutika Tanganyika. Short of that Muungano uliopo una walakin na walakin huo ulisababishwa na Nyerere na Karume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…