Nimeona mabadiliko ya hotuba za Lissu hivi karibuni kama ifuatavyo:
1. Hoja zinasemwa haraka haraka na muda hautoshi.
2. Hoja kadhaa muhimu hazina ufafanuzi wa kutosha.
3. Tundu Lissu na CHADEMA wameacha kuongelea tukio lake la kupigwa risasi nyingi.
Umuhimu wa haya mambo matatu ni huu ufuatao:
1. Ingawa Lissu anaendelea kuvutia, alikuwa anatuvuta zaidi kwa kutuelezea jambo taratibu hadi mwisho wake akiwa (deliberate and comprehensive). Ikiwa kufanya hivi kunachukua muda, achague hoja muhimu mbili tatu tu kwa kila mkutano azieleze vizuri, na zingine ndizo azisemee haraka haraka. Abadilishe mpangilio huu kila mkutano.Pia waandaaji wahakikishe kuwa anapata muda wa kutosha. Wagombea ubunge au wenyeji wake waombe kura kwa haraka na wamuachie muda. Kama wenyeji wake wamejiandaa, wanaweza kupewa muda zaidi waelezee hoja mojawapo ya Lissu kwa ufasaha, naye asiirudie kwenye mkutano huo.
2. Hoja zinazorudiwa sasa ni wafanyakazi kutopewa nyongeza ya kisheria, kutopandishwa madaraja, kujenga uwanja wa Chato, Kupeana miradi na kuilipia kifamilia, wananchi wa kawaida kulipishwa tozo hata kwa mauzo ya chakula cha siku tu, wavuvi kunyang'anywa nyavu au kuuawa, wafanya biashara kulipishwa kodi zaidi au kufilisiwa, na kutishiwa au kubambikiwa kesi, hasa kwa wakosoaji wa serikali. Mengi ya haya yanajieleza, na Lissu ameendelea kuyajumuisha kuwa wananchi wamepata mateso kila mahali.
Hili jumuisho ni muhimu sana, asichoke kulisema. Yako majumuisho kadhaa ya Uwanja wa Chato: utawala wa kifalme, ubaguzi, kipaumbele kibovu, kuvunja sheria ya manunuzi, na ubadhirifu. Hivi ni vipengele muhimu vinavyohitaji si sekunde bali dakika kadhaa kuvielezea. Kila mojawapo inaweza kufafanuliwa kwa kina. Kwa mfano, Lissu anaweza kupiga hesabu akawaambia wasikilizaji ni zahanati au maji au bima ya afya au huduma kiasi gani kwa wakulima ingelipiwa na pesa za kiwanja cha Chato. Na mlinganisho huu ni mzuri hata kwa ununuzi wa ndege-ulaya nyingi.
3. Tundu Lissu alimwagiwa risasi za kumuua zaidi ya 30, zikamwingia 16, akatibiwa kwa miaka mitatu. Alinyimwa malipo ya tiba yake aliyostahili, alifutwa ubunge kibabe, amekosa mafao yake kibabe. Ni uonevu usioelezeka. Usemwe, hata uimbwe! Siyo wa kuonea aibu! Kama Lissu anashindwa kulisemea yeye binafsi tunaelewa, basi atafutwe mtu mahiri kila mkutano mwanzoni au mwishoni aliseme vizuri, siyo haraka haraka kutimiza mradi, bali kwa hisia na huzuni. Awaguse watu.
Yeye Lissu au mtu mwingine atukumbushe kila mkutano kuwa wengi tuna mikasa ya uonevu kama ya Lissu. Msichoke wala kuona aibu. Wala msisikilize wanaowadanganya kuwa hiyo si sera eti ni kutafuta huruma. Hiyo ni sera kubwa ya kuhitaji utawala bora usio na uonevu wala jaribio la mauaji. Wala msiridhike kuwa wananchi wameshaelewa. Semeni tena na tena (hata kwa maneno tofauti lakini ujumbe ule ule).