LGE2024 Tundu Lissu: Wagombea wetu wengi wamewekewa mapingamizi kabla hata majina yao hayajabandikwa

LGE2024 Tundu Lissu: Wagombea wetu wengi wamewekewa mapingamizi kabla hata majina yao hayajabandikwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Tundu Lissu akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Singida amesema wagombea wao wengi waliwekewa mapingamizi hata kabla ya majina yao kubandikwa

Singida tulisimamisha wagombea takriban 1225, wamepigwa mpaka tuliobaki nao nafikiri hawafiki 500 zaidi ya nusu wameondolewa pamoja na kwamba kanuni zinasema mapingamizi yataamuliwa ndani ya siku mbili tokea mapingamizi hayo yapokelewe.

Mapingamizi yalitakiwa yapokelewe tarehe 9 na tarehe 10 Novemba. Mapingamizi mengi yameletwa tarehe 8, kwa mujibu wa kanuni, tarehe 8 ilikuwa siku ya kuteua wagombea tu.

Ukishabandika majina saa 2 mpaka saa 10, kesho yake saa 2-10 na siku inayofuata saa 2-10 ndiyo wakati wa kuweka mapingamizi.

Wagombea wetu wengi wamewekewa mapingamizi kabla hata majina yao hayajabandikwa ukutani sababu majina yalibandikwa tarehe 8 kuanzia saa 2-10, hao walioweka mapingamizi tarehe 8 hiyo hiyo walijuaje matatizo ya hao wagombea waliowawekea mapingamizi?
 
Mliposhiriki uchaguzi mlitegemea nini

Ova
 
Back
Top Bottom