Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Walimu wote tutawainua

MOSintel Inc

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2016
Posts
817
Reaction score
593
"Mfumo wetu wa Elimu lazima uondokane na habari ya kufaulu mitihani pekee na utengeneze Watoto wenye maarifa, tutafanya mabadiliko makubwa kwenye Elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya Walimu ambao wameteseka miaka nenda rudi "-Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu akiwa Tabora leo

"Walimu wetu ndio Watu wa hali ya chini kuliko Watu wengine wote miaka nenda rudi, huwezi kutengeneza Elimu wakati Mwalimu anadharaulika, Walimu hakikisheni CHADEMA tunashinda ili muondokane na hali hii ya kupuuzwa"- LISSU

"Sheria za Nchi zinasema ni haki ya kila mfanyakazi kupata nyongeza ya mshahara ili aendeshe maisha ila ni miaka 5 sasa yanajengwa Madaraja, SGR na zinanunuliwa Ndege, wafanyakazi hawajaongezwa mishahara, wameonewa kiasi cha kutosha, mwaka huu semeni sasa basi"-Lissu akiwa Tabora

Source: #MillardAyoUPDATES

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…