SI KWELI Tundulisu kawadhikaki walimu ambao hawana ajira

SI KWELI Tundulisu kawadhikaki walimu ambao hawana ajira

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekutana na taarifa chanzo Millard ayo inayo sema mheshimiwa Tundulisu kawadhikaki walimu ambao hawana ajira 👇👇👇

Je ni kweli?
JAMII CHECK_SIKWELI_24FEB25 (2).jpg
 
Tunachokijua
Hivi karibuni kumeibuka umoja wa walimu wasio na ajira Tanzania ukijulikana kwa kifupi kama (NETO). Umoja huu umefanya mkutano na waandishi wa habari Februari 21, 2025 na kuelezea mambo mbalimbali yanayowasibu wao kama walimu wasio na ajira na kutoa mapendekezo yao kwa Serikali. Tazama hapa.

Madai

Mdau wa JamiiCheck.com amehitaji kupata uhalisia wa taarifa inayodai kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewadhihaki walimu kuwa hawajitambui. Taarifa hiyo imeambatana na screenshot inayoonesha kuwa Lissu amechapisha katika ukurasa wake wa X akiwashauri wazazi wasikubali watoto wao kusomea ualimu kwani kufanya hivyo unamuandaa mwanao kuwa mpumbavu na mtumwa kwa maisha yake yote.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Lissu hajachapisha maneno hayo katika ukurasa wake wa X zamani Twitter.

Screenshot hiyo inayosambazwa ni ya kughushi na haina uhalisia wowote kwani haipo katika ukurasa rasmi wa mtandao wa X wa Tundu Lissu. Lissu alichapisha kwa mara ya mwisho katika ukurasa wake wa X Februari 21, 2025 akitoa taarifa ya kukutana na viongozi wa ACT-Wazalendo ofisini kwake. Tazama hapa.

Kwa upande wa grafiki ambayo inaonekana kuwa ni ya Millard Ayo, ufuatiliaji umebaini kuwa grafiki hiyo haijatolewa wala kuchapishwa na Millard Ayo hivyo si halisi.
Ni ukweli ndani ya upotoshaji wa wadau
 
Lisu mwenyewe aje kukanusha taarifa hii la sivyo tutandelea kuamini kuwa yeye ndiye aliyeichapisha.

Mwalimu uhurumoja uko wapi.
 
Back
Top Bottom