KERO Tunduru: Vyama vya Msingi vinachelewesha malipo ya wafanyabiashara wa mazao

KERO Tunduru: Vyama vya Msingi vinachelewesha malipo ya wafanyabiashara wa mazao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tabia hiyo inatajwa kuwa endelevu kwa vyama hivyo kutolipa kwa wakati pesa za wauza mazao hao. Minada inapigwa kila wiki ndani ya wilaya hiyo lakini malipo ya pesa katika mnada husika hazilipwi na kupiga mnada mwingine ambao unashuka bei.

Wilaya hii imekuwa tofauti na wilaya nyingine zilizopo mkoani Ruvuma kama Namtumbo ambapo wanalipa kila mnada kabla ya mwingine kwa wakati.

Inasemwa kuwa kama wanakaa na pesa kwa muda mrefu basi watoe gawio katika pesa hizo ikidhaniwa kwamba zipo Katika mzunguko kwakuwa pesa huwezi weka ndani.

Pia soma
- DOKEZO - Tunduru: Vyama vya Ushirika vinawadhulumu na kuwaibia pesa wakulima wa ufuta

IMG_20240225_092959_238.jpg
 
Back
Top Bottom