Tungekuwa na Katiba kama ya Kenya tungefika mbali

Tungekuwa na Katiba kama ya Kenya tungefika mbali

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Katiba ya sasa ya Kenya ilipunguza kwa kiwango kikubwa sana vyeo vya kugawa kama Karanga.

Katiba ya Kenya bado naamini ni moja ya katiba bora Africa na ni nchi chache Africa zina katiba ya aina ile.

Ndo maana hadi Majaji au IGP wa police Kenya anatuma maoumbi, Mkaguzi mkuu wa hesabu anatuma maombi ya kazi hio.

Hii nchi baada ya miaka 60 ya Uhuru ndo kwanza tuna speed ya 5g kwenye kugawa vyeo kama karanga.

Hakuna mfumo wa kurithishana kazi mfano watumishi wa Umma kwba ndo wapabde ngazi waje kuwa wakuu wa wilaya, mikoa au Wakurugenzi, hapana.

Gharama za kuhudumia hawa ni kubwa sana, Fikiria wale walio achwa kwenye hizi teuzi za kugawa kama pipi inabidi wagharamikiwe kurudishwa makwao na walipwe viinua mgongo vyao.

Hawa wapya inabidi wasafiriswe wao na Familia zao hadi maeneo yao ya kazi mapya hapa ni pesa za kutosha zinatumika.

Vipi kama mfumo ungekuwa kwa kila wilaya watunishi wanapanda kuwa wakuu wa wilaya au Mkoa au Mkurugenzi? Unazani tungeokoa kiasi gani kusafirisha wateuliwa?
 

Hamia Kenya!

Hivi ulikuwa na umri gani Kina Lissu walipopewa nafasi ya kututengenezea Katiba na badala yake wakawa wanamtukana na kumkashifu baba wa taifa JKN?

Tulipoteza mabilioni ya fedha kama nchi, na badala ya kupata katiba, matokeo yake tukapata ukawa usio na tija!
 
Ina impact yeyote kwa maisha ya Mkenya hiyo katiba?

Watu ni masikini, ufisadi ndio usiseme, sasa katiba yao nzuri inawasaidia kitu gani?

Katiba nzuri ni ile inayoleta mfumo wa mzuri wa kuwaletea watu maendeleo.

Hapa kwetu mijitu inataka katiba mpya! Ukiuliza kwanini unataka katiba mpya unaambiwa ni ili kuweka mazingira ya chadema kushinda.

Upuuzi mtupu,!
 
Ma ccm tunapaswa kuyatoa nduki na mawe nchi mzima tuamasishane siku moja nyingi sana.
 
Tatizo wasomi Watanzania wanalea ujinga na Vyama mbadala navyo haina muelekeo wa kitaifa bali umimi.

Kenya wamefikia hapo kutokana na msukumo wa Vyama mbadala na wasomi wa nchi hiyo.

Wakwetu ndio hao , ma Prof Kapuya, Mwandosiya Muongo nk.
 
Nchi hii ukishashiba basi huoni tena kama kuna shida na katiba bali ukiwa nje ya mfumo ndio unaona katiba inashida. Hata wewe kesho ukiwa mkurugenzi wa jiji I SWEAR HUWEZI KUENDELEA KUDAI KATIBA MPYA. (UBINAFSI).
 
Back
Top Bottom