Tungo: Hatoki karibu yako pindi ukiwa na hela

Tungo: Hatoki karibu yako pindi ukiwa na hela

nentewene

Senior Member
Joined
Jun 9, 2017
Posts
144
Reaction score
94
Hatoki karb yako, pale ukiwa na hela.
Ataacha chokochoko, penzi lote utapewa.
Hata ukiwa mnoko, sifa tele wamwagiwa.
Utapata madikodiko, na mapenzi utalewa.
mke atakuelewa pindi ukiwa na hela.

Utaliona sokomoko, pindi ukiishiwa.
Tena utakua kituko, na talaka utapewa.
Utaitwa mbwa Koko, au mwanaume hewa.
Mke atakuelewa pindi ukiwa na hela.

Moto utawaka..nyumba itakua jela.
Patakua patashika.. tena atakukera.
Kila muda atafoka...yote sababu ya hela.
Mke atakuelewa pindi ukiwa na hela.

Wameshindwa wamanga, wenye rangi na sura.
Six pack zimejipanga, tena wameshiba kula.
Sasa mwenzangu kiranga, mwenye sura kama chura.
Kwa maneno yakaranga, natumbo limefura.
Yamekujaa majanga na ugumu wasura.
Hebu jarib kujipanga..utafute mahela.
Mke atakuelewa pind ukiwa na hela.

Sio ufundi kitandani, utafnya apagawe.
Wala sio gemu ndefu, itamfanya alewe.
Wala sio uzoefu, nakucheza kama pele.
Mpe mke pesa.. nauache kelele.
Kweny mapenzi utatesa ..watu wataona gere.
Hebu mpe sasa.. uchezewe segere...

  1. Tungo: wafatuta shotikati
  2. Tungo: Leo utahonga laki, kesho atataka dola
 
Bonge moja la shairi,hongera.Najiangalia kwenye kioo mpaka tutone tunatiririka kutoka kwenye macho .
 
siku ya jumapili, maskani niliketi.
kwa macho yangu mawili, nikifanya utafiti.
akapita kimwali,tena alikua fiti.
alikua pisi kali, rangi yake chokoleti.
sifa anastahili, yuko vizuri pale kati.
ilikua sinza mori, kumbe anasaka noti.
tena wala hajali, tena amejikoki.
asofanya ya halali, kwa kutafuta shotikati.
 
leo utahonga laki, kesho atataka dola.
ukimnunulia mishkaki, atadai na kijora.
yani hawasomeki, ni nyingi zao hila.
michekupo hawaridhiki, zitaisha zako hela.

utampeleka samakisamaki, ila nyumbani hawajala.
utamkodia pikipiki, ila mkeo daladala
utampeleka denimaki, kama mtoto wa kajala.
mwisho utakua dodoki, na atakufanya fala.
michekupo hawaridhiki, zitaisha zako hela.

utalala kwake wiki, ila bado atazila.
utampa kadi ya benki, bado atadai dira.
ukijifanya fulubeki, atakuchezea mpira.
achune zako steki, ubakie na kipara.
michekupo hawaridhiki, zitaisha zako hela
 
Back
Top Bottom