Tungo: Nipeni ushauri, mke gani nichague

nentewene

Senior Member
Joined
Jun 9, 2017
Posts
144
Reaction score
94
Naombeni ushauri, mke gani nichague!
Niangalie uzuri, mtaani wanijue?
Au anaeweza shughuli, kitandani nitulie.
Au alietulia tuli, pekeangu nitanue.
Ebu nipeni ushauri, leo hii nijue.

Nichukue mwenye tako au mwembamba anatosha.
Nichague mwenye cheko, anaeweza kunikosha.
Au nichukue mnoko, anaejua kukiwasha.
Au anaejua jiko, aje kunishibisha.
Mie nataka mwenye mshiko, anipe raha za maisha.
 
Inaonekana mkuu mtaalamu wa vigodoro
 
Hivi mkuu ni kweli ndio unatuuliza mambo kama haya..? Sasa mungalie mke wa baba yako sifa zake halafu fuata nyayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…