Emanuel Eckson
Member
- May 24, 2017
- 11
- 14
Serikali ya Tunisia imeidhinisha hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa mgombea urais wa nchi hiyo kwa mwaka 2019, Nabil Karoui pamoja na kaka yake ambaye ni Mbunge, Ghazi Karoui kwa kosa la kuvuka mpaka wa nchi hiyo kwa njia haramu (pasipo vibali) hali iliyopelekea kukamatwa kwao na kuwekwa kizuizini siku ya jumatatu Agosti 30, 2021 nchini Algeria.
Taarifa ya kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwao imetolewa jana Agosti 31, 2021 na Msemaji wa Mahakama ya Kasserine ya nchini Tunisia ikiwa ni siku moja tu tangu kutangazwa na vyombo usalama vya nchini Algeria kama inawashikilia viongozi hao.
Msemaji wa Mahakama hiyo amenukuliwa akisema “Hati ya kukamatwa kwa Nabil and Ghazi Karoui zimeidhinishwa kwa makosa ya kuvuka mpaka wa nchi hiyo kwa njia haramu.”
Pia, imeelezwa kuwa mtu aliyewasaidia viongozi hao wa chama chama cha Qalb Tounes kuvuka mpaka huo bila vibali ameshakamatwa na polisi.
Aidha, ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2019 Bw. Nabil Alikuwa mpinzani wa karibu wa Rais wa sasa wa nchi hiyo, Kais Saied na kufanikiwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais huyo.