Pre GE2025 Tuombe Mwaka 2024 Uwe ni Mwaka wa Mageuzi ya Kweli ya Kidemokrasia ya Kweli Tanzania. Tume Huru, Uchaguzi Huru na wa Haki! Happy New Year!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mr
Mr Pascal Mayalla siku zote nakuona kama msanii mwenye maneno mengi mtu akisoma headings zako anaweza kudhani unamaanisha unachokiomba au kukisema lakini mambo yakienda sivyo bado utapongeza uharibifu. Hatutasahu rangi yako halisi wakati wa magufuli!!!! (Ulianza vizuri ulipomuuliza swali pale ikulu ila alipovurunda ukavurunda nae. Hatutasahu rangi yako halisi wakati wa shambulio la lisu.
 
Nini kifanyike? CCM ndiyo inataka ukate tamaa iendele kuweka watu wabovu, lazima tuukatae huu mfumo ovu wa kuwepo na nyumba za tembe Tanzania mpk leo
Mkuu kwenda kushiriki upumbavu nawe utaitwa mpumbavu ni bora uache wapumbavu wazidi kuonesha upumbavu wao.kuna maana gani ya kwenda kuchoma muda kwenye mistari ikiwa tayali mshindi kasha julikana.

Binafsi siwezi piga Kura ndani ya taifa Hili,hata katibu mstaafu wa CCM DK.Bashiru kasha wahi sema "watu wenye akili timamu washa lipuuzia sanduku la Kura"

Kanuni ni zile zile muache mpumbavu na upumbavu wake.Mwl.Nyerere kasha wahi sema
"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake"

CCM kumejaa wapumbavu.
 
CCM ndiyo wanataka watu kama wewe, mimi nitashiriki kwa kupambana nao CCM
 
Watanzania wengi wameshajikatia tamaa wanajua wakipigia kura wanayemtaka hatangazwi. Ni Kama kupotezewa mda wa kupanga foleni
Mkuu hawajakata tamaa, bali wamelipuuza box la kura. Kuna tofauti kubwa ya kukata tamaa na kupuliza.
 
Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi hakutakuwa na mabadiliko ya kweli. Kuendelea kushiriki hizi chaguzi za kihayani ukitegemea mabadiliko ya kweli ni kupoteza muda.
 
Pascal buana! Hivi huwa unaandika haya Ukiwa na akili timamu? Au unakuwa umelewa pombe?

Tume huru itoke wapi?
 
Pascal buana! Hivi huwa unaandika haya Ukiwa na akili timamu? Au unakuwa umelewa pombe?

Tume huru itoke wapi?
Mkuu Mkulima , Watanzania ni watu wa ajabu sana, full kulalamika with negativity!. Muswada wa kurekebisha sheria ya uchaguzi na tume ya uchaguzi imeisha somwa kwa mara ya kwanza mmepewa fursa toeni maoni yenu, hamtoi, unauliza tume huru itoke wapi!.

Unamaanisha sisi tunao amini tunakwenda kupata Tume Huru na Shirikishi ya uchaguzi, ni tumelewa!.
P
 
Hiyo sheria mpya ya uchaguzi ni kiinimacho.

CCM wanayajua maanguko yao makubwa ni katiba mpya na tume huru.

Katiba mpya itaruhusu sisi kuchallenge matokeo ya urais kortini kitu ambacho hakifanyiki sasa ambapo genge la watu wachache ndio wanapanga na kuamua rais awe nani.

Tume huru italeta mtu asiyeyumbishwa bali anasimamia na kubanwa na sheria tuliona vile Wafula Chebukati wa IEBC aliyosimama kwenye chaguzi ya jirani ile ndio inatakiwa sasa bongo.

Sio hii michezo ya CCM kujaza maaskari wanaingiza kura na watu wengine wanaingiza kura za mabunda kwenye vikapu na mabegi
 
Paschal, hii ilikuwa mada yako ya kufungia mwaka. Nina uhakika uliiandika ukiwa umelewa, au umeshiba sana. Maana haiendani na Ile Imani yako ya ccm kutawala milele. Ili ccm itawale milele lazima katiba ya nchi, na tume ya uchaguzi viwe vibovu ili ccm iibe kura kama wanavyotaka. Bila wizi wa kura paschal unajua kabisa ccm haina ushawishi kwa wananchi.
 
Bila machafuko
Watanzania ni watu pisi sana, hatuna watu wa machafuko type.
ama mapinduzi ya kijeshi
Jeshi la Tanzania ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania, TPDF or JWTZ, hivyo sio Jeshi la kufanya mapinduzi
hakutakuwa na mabadiliko ya kweli. Kuendelea kushiriki hizi chaguzi za kihayani ukitegemea mabadiliko ya kweli ni kupoteza muda.
Naomba tuu niheshimu mawazo yako.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…