Tuongee fact: Kwa style Taifa Stars itaendelea kuwa team ya mabonanza.

Anselm

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
1,710
Reaction score
291
Tokea wenye dhamana ya kuendesha mpira wa miguu wa Tanzania walipomteua Salum Mayanga kuwa kocha wa team ya Taifa nilipoteza imani kabisa na team hii pendwa na Watanzania wote bila kujali mapenzi yetu kwa vilabu vyetu.
Nikiwa kama mtu wa mpira kamwe ckuwahi kupumbazwa na matokeo ya mashindano ya COSAFA ambayo team yetu ya Taifa iliibuka kama mshindi wa 3,kwakuwa nilijua yale mashindano ni kama bonanza tu ambapo team zote shiriki ukitoa ya kwetu zilipeleka Wachezaji wa vikosi vyao vya 2 na wengine wenye program endelevu za soka vya 3 na vya 4,yaani kwaufupi hakuna team iliyopeleka team wanazozitumia kwenye mashindano yanayotambuliwa na CAF au FIFA ukitutoa sisi na ndo maana kwetu ilikuwa ni rahisi kuonekana tunapata matokeo.
Sasa niende kwenye hoja 1 kwa 1 kwanini ninamuona Mayanga kama mmoja kati ya makocha watakao'fail zaidi ktk hili jukumu alilopewa:-
1. Ni aina yake ya uteuzi wa team,ni ya kushangaza na sijapata kuiona toka nimeanza kufatilia masuala ta uteuzi wa team za Taifa.
Duniani kote team za Taifa hubebwa na wachezaji waliokomaa kimashindano na kuthibitika kuchangia matokeo mazuri ya Club wanazotoka,huwezi kumtegemea Boko akuletee matokeo wkt kwa kipindi kirefu alikuwa majeruhi kwahiyo bado hajarejea kwenye fitness yake ya kawaida,au kutupangia team inayotegemea ushambulizi wa Stamili Mbonde ni kututania Watanzania,huyu Stamili Mbonde amefunga magoli mangapi kwenye ligi yetu ya ndani kiasi cha kutufanya tumwamini kuwa atatufungia magoli kwenye international games,hiv kweli mchezaji anayeshindwa kuzifunga Ndanda na Majimaji ndo Mayanga anataka amtumie kuzifunga Rwanda na The Cranes ya Uganda?
Kwenye Ligi iliyomalizika kuna wachezaji wengi walioonyesha walau wana mbinu za kufunga licha ya kuwa walikuwa kwenye vilabu vidogo,watu kama Abdulhaman Mussa(mfungaji bora sambamba na Msuva),Rashid Mandawa,Kelvin Sabato na Omari Mponda wangejumuishwa wangeweza kutupa kitu cha tofauti na hao akina Boko wake. Hata Ibrahim Ajibu angekuwa na mchango chanya zaidi kuliko baadhi ya hao washambuliaji alio nao kwenye team.
2. Upangaji wa team/kutokuwa na uwezo wa kusoma mchezo na kufanya Sub stahili (Super Sub) ni moja ya weakness zake nilizoziona anzia kwenye COSAFA mpk kwenye mechi ya jn,mtu unaona kabisa kuwa team imepoteza mwelekeo kwenye kiungo na mbele,una wachezaji wenye uwezo wa kucheza nafasi hiyo na wazuri hata kwenye kufunga lkn huwatumii kabisa,ukiuliza utaambiwa falsafa,falsafa gn ya kipuuzi hivyo...
3. Kutojua atumie wachezaji gn kwenye mashindano gn: Anakwenda kinyume kabisa na makocha wenzake,badala ya kupeleka vijana wa Serengeti Boys wengi kwenye COSAFA yeye kapeleka full mziki hlf kwenye CHAN ndo anakuja kuwajumuisha hawa watoto tena wakiwa wametoka kwenye mapumziko ya muda mrefu,hlf Watanzania tunataka tuamini kuwa aina hii ya utumiaji wa wachezaji itatupeleka CHAN,its none sense.
4. ...........
Ngoja niishie hapa kwanza,J2 njema watu wenzangu wa mpira.
 
Nimeona gazeti la mambumbumbu fc limeandika eti ""wachezaji stars wastushwa na matokeo ya sare ""
 
Kocha sikiliza ushaur wa wadau hii kitu inatuumiza sote. Chukua vijana hawa waliotajwa hata kama hawajatokea simba au yanga wataisaidia nchi na ww utaonekana bora. Kha!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwanini msuva na kichuya wanapata namba hapo stars!?
 
Tushasema saana pale hamna timu wala mwalimu na tusipovunja Ile timu tumekwisha....nimesikitika saana kuona timu yangu ya Simba ikiendelea kusajili vibonde kutoka kwenye hiki kikosi
 
Hatuna programu za kuendeleza soka la vijana.

Kibaya zaidi wameteua kocha asiyekidhi vigezo. Nchi yoyote huchagua kocha mzalendo kutokana na matokeo yake uwanjani kwenye ligi zao.

Mayanga ana mafanikio gani kuwazidi makocha wengine Wazalendo?
 
 
Hii Nchi kuna madudu sana, JPM mpira ni kiwanda kikubwa sana tilia mkazo eneo hili. Unaweza zalisha ajira kwa wingi sana, tuletee waziri kijana mpenda michezo, najua wapo wengi mno, huyo mwakyembe muache afundishe sheria huko. Huku Kwny michezo tunataka watu makini ajira ni nyingi mno na fedha za kigeni pia zipo huku kwnye soka, niteue kuwa hata katibu mkuu hapo wizarani nifanye Mapinduzi ya michezo yote nchini sitakuangusha.
Toa kodi Kwny vifaa vya michezo, ingiza wawekezaji kwny michezo hasa shule za michezo, mashirika ya mifuko ya jamii watujengee viwanja vitano nchini, tuandae African cup of nation, viwanja vinavyomilikiwa na ccm rudisha serikali, ajiri makocha wa kigeni huku panalipa jamani, khaa

Sent from my GT-N5100 using JamiiForums mobile app
 
Hatuna programu za kuendeleza soka la vijana.

Kibaya zaidi wameteua kocha asiyekidhi vigezo. Nchi yoyote huchagua kocha mzalendo kutokana na matokeo yake uwanjani kwenye ligi zao.

Mayanga ana mafanikio gani kuwazidi makocha wengine Wazalendo?
Kuna kocha anaitwa Julio, japo binafsi simpendi lakini angepewa Stars naamini angeweza kufanya vizuri kuliko huyu anayejiita Ma_Yanga huku akiwa amejaza machezaji Ma_Simba.

Stars ni timu ya mabonanza kwani wachezaji wengi wametokea huko kwenye mabonanza ya M_Simba_zi!
 
Mayanga mshamba...dunia ya sasa unapanga mawinga wawili nani anafanya hivyo..tukitaka matokeo Rwanda ,back line ibaki kama ilivyo namba nane acheze Ndemla,kulia Mzamiru,kushoto Hoza na sita Himid...Boko na Rapha wasimame mbele.tunakuwa na typical midfielders watano lazima tutawazidi maarifa..
 
Mm bado nampata benefit of doubt kwa sababu hadi sasa hajafeli chochote kulinganisha na makocha waliopita. Nikukumbuka upuuzi uliofanywa na Mart Nooij ambapo Taifa Stars iliondoshwa kwenye mashindano haya haya ya bonanza bila kufunga hata goli la offside naona afahdali Mayanga kaleta kitu kipya. Stars hiyo ilikuwa inapigwa 3 kila mechi!

Mkwasa alikuwa na wachezaji wote hao wazuri na wazoefu lakini akatuletea aibu ya kufungwa 7-0 kitu ambacho hakijatokea kwa zaidi ya miaka 50!!! Aidha kipindi chake timu ikaendelea kushuka kila kukicha

Huyu Mayanga amesababisha Tanzania imepanda kwa kasi kwenye viwango vya FIFA, it's fair kabisa kusema amefanikiwa maana hizi ndio facts.

Pamoja na yote kuna makosa anafanya kama binadamu wengine au makocha wengine waliopita - kuchagua wachezaji fulani na kuacha wengine. Katika nchi kuna wachezaji wengi sana hivyo si rahisi kuwaridhisha wote na hivyo tumwachie mwenyewe afanye vile aonavyo vema. Tutamkumu kwa matokeo lakini kwa sasa bado ni mapema sana labda inatosha tu kumpa angalizo.

Nilisema toka zamani, tatizo la Mayanga sio uwezo ila kwa kuwa hajawahi kuwa kocha wa Yanga au Simba!!!!!! Ukweli huu ndio unaomwandama maana hakuna ambacho mashabiki wanazi wa hizi timu wanachojua zaidi ya kuamini mchezaji mzuri na kocha mzuri ni kutoka kwao tu.

Tatizo jingine ni kuwa Yanga wengi wanaona kuwa sasa hivi hawana wachezaji wengi ktk kikosi ktk timu ya Taifa. Watafanya kila wawezalo kumharibia Mayanga bila kujiuliza maswali magumu ya kwanini achague wachezaji kutoka timu hii ambayo imeshuka kiwango kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na Yanga ya 2015/2016. Ukweli ni kuwa hakuna kocha yeyote makini asiyesukumwa na mapenzi anaweza kuchagua wachezaji angalau 3 kutoka Yanga kuingiza timu ya Taifa. Na sababu ziko wazi sielewi kwa nini watu hawazijadili

1. Wachezaji wengi walioko kikosi cha kwanza cha Yanga ni wageni. Niyo, Tambwe, Chirwa, Bosuou, Ngoma, Kamusoko.
2. Waliobaki wazawa ni MSUVA pekee ndio aliyekuwa fomu na hajawahi kuachwa timu ya Taifa
3. Yondani umri, Cannavaro na Mwinyi, kwanza kwa sasa ni wachezaji wa Zanzibar Heroes na pili viwango vyao sio bora kuliko walioko stars

Bila kupepesa macho hata Ramadhani Kessy bado sio mchezaji wa daraja la juu ukilinganisha na Juma Abdul ambaye kwangu mimi huyu ndio anapaswa hata kuchukua namba ya Kapombe kabisaaaa. Anayestahili kuwa Stars kwa sasa ni Msuva, na Juma Abdul kama amepona.

Kuhusu Ibrahim Ajibu hapa ndio unaona watu walivyo wanafiki. Ajibu ameachwa toka akiwa Simba hakuna Yanga aliyelalamika, sasa hivi hata kabla hajacheza mechi moja tayari watu wanapiga kelele

Hoja kuwa wachezaji bora ktk Ligi kuchaguliwa timu ya taifa nadhani hili limefanyika lakini watu wajue haiwezekani kuchaguliwa wote. Mbaraka Yusufu na Shaaban Iddi Chilunda ndio wachezaji waliowika na wamechaguliwa ila wamepata majeruhi, na hili sio kosa la kocha. Sasa isingewekana achague stikers 5 tu ili mradi kuaccomodate kila mchezaji aliyefanya vizuri.
 
Tatizo siye watu wenye akili kama wewe mwenzangu tumebaki wachache sana. Katika 1000 unaweza kuta tupo wawili tu. Wengi ni aina hii ya mleta mada.

Umeelezea vizuri ngoja waje jamaa wale

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…