kimbomba25
JF-Expert Member
- Jan 27, 2017
- 1,160
- 2,117
Tanzania iko kwenye tanzia, ikiomboleza kifo cha tozo-stahimilivu na kufufuka kwa tozo-kandamivu kwenye miamala ya mitandao ya simu.
Naam, tumefikia zama ambazo ukiona meseji ya M-pesa inabidi usonye na kumlaumu mtumaji kabla ya kuifungua. Yote hiyo ni kukwepa makato makubwa ya tozo za miamala. Kila kona ni kilio, si kwa mafakiri wala wakwasi.
Kwanza, napingana na hoja nzima ya kutafuta mbadala, kwa kuwa sikubaliani na suala la kutafuta ‘njia mbadala’ ilhali ‘njia kuu’ inapitika na haina changamoto. Naam, ya nini tupite ‘service roads’ ilhali ‘main roads’ zikiwa nyeupe kabisa? Ninachomaanisha ni kuwa, hatuwezi kuikimbia mitandao na kutumia njia mbadala ilhali hakuna changamoto yoyote zaidi ya tozo. La msingi tozo ziondolewe ili huduma zirejee kama ilivyokuwa awali. Tena ikiwezekana zipunguzwe zaidi ya awali ili maisha yawe bora kwa kila Mtanzania kama kauli-mbiu za viongozi zinavyodai.
Ninapingana na hoja ya kutafuta mibadala kwa sababu ni hivi; inasemekana tunatozwa hivyo ili fedha zitumike kujenga zahanati na vituo vya afya. Kama lengo ni kujenga zahanati kupitia tozo, basi hatuwezi kulikimbia hilo kwa kuacha kutumia mitandao, kwa maana tukikimbia huku, watatufuata kule, hadi lengo lao la kujenga zahanati litakapotimia.
Naam, hivi tunadhani lengo lao la kujenga zahanati litakufa kwa sababu tu hatutatumia mitandao? Hapana! Wao wanatafuta penye upenyo wapige, mkikimbia huku, watawafuata kule hadi kieleweke.
Kuhama maana yake tumekubali mabadiliko. Hii haijakaa sawa, kukubali kitu chenye dosari inaonesha ni kwa namna gani tulivyo ‘tepetevu’, na kwa hivyo hata huko tutakapokimbilia wataweza kuleta shida, na badala ya kupambana tutahama. Sasa tutahama hadi lini? Hapo ndipo Sioni haja ya kuwakimbia huku. Tuumane nao jino kwa jino waondoe tozo na maisha yaendelee huku tukiendelea kuwakumbusha kuwa hii ni huduma na si anasa.
Japokuwa kuongeza tozo kwenye miamala ya simu na kutokuongeza tozo kwenye miamala ya kibenki kunaibua maswali lukuki, tuachane na hilo kwa wakati huu!
Watanzania wenzetu wengine wanajitahidi kutuaminisha kuwa hizi tozo ni rafiki na tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi. Wanatakiwa watambue sisi si washamba na mazuzu, tunafahamu umuhimu wa kulipa kodi, lakini kodi kandamizi hazina manufaa wala hazitaleta maendeleo. Watu wataacha kutumia mitandao kabisa, hapo kutakuwa na hasara mbili mtawalia, kwanza serikali itakosa mapato, pia biashara za watu zitakufa. Kuna maana gani sasa? Kadiri kodi zinavyokuwa stamilivu ndivyo ambavyo watu wengi watavutiwa kutumia huduma, hivyo kupata kidogokidogo kutoka kwa wengi kutaleta mapato mengi.
Chambilecho wahenga, haba na haba hujaza kibaba, sasa serikali tukufu haijui hili. Ikiona watu wengi wanafanya biashara basi huamua ilete tozo kubwa ili ikikusanya itajirike haraka. Matokeo yake watu wanaacha kutumia. Hasara mara mbili. Hata wanaposikia kumefanyika miamala ya mabilioni ya fedha huwa hawafikirii kuwa ni hizi elfuelfu ambazo watu hutumiana ndizo huleta mabilioni.
Haijakaa sawa!
Watu wanapendekeza njia mbili kuu za kukwepa tozo za mitandao; benki na kutumia mabasi.
BENKI
Kwanza, kama chanzo cha mapato ni tozo za miamala, maana yake watu wakikimbia miamala ya simu wakahamia benki, watozaji watawafuata hukuhuko kuwatoza. Hivyo sioni nafuu.
Ukiachilia yote hayo, mazingira ya kibenki ni magumu kwa Watanzania wengi. Kuna mawakala wangapi wa benki nchini ukifananisha na wamakala wa mitandao ya simu? Hili la benki angalau linatekelezeka kwa mazingira ya mijini, lakini vijijini ambako ndiko kuna watumiaji wengi zaidi hali ni mbaya. Matawi mengi ya benki yapo mijini, je, watu watakuwa wakitoka vijijini na kwenda mijini kufanya miamala. Mfano mtu atoke kijijini ili akatume ‘pocket money’ ya mwanawe shuleni ya shilingi 10,000? Ama mtu afunge safari kilometa ishirini ili akatoe shilingi 5,000. Ni ajabu!
MABASI
Wengine wanapendekeza tutumie mabasi, ima kwa kutuma kwa kupitia makondakta ama sisi tupeleke na kuzifuata fedha kwenye yale maeneo ambayo nauli yake iko chini ukilinganisha na tozo za miamala.
Hii njia licha ya dosari zake nyingi lakini ni kichekesho. Inachekesha kuwa tunataka kurudi zama za mawe. Pindi dunia ikipiga hatua kwenda mbele, sisi tunapiga hatua kurudi nyuma. Watu wanaingia kwenye cryptocurrencies, sisi tunawaza kutumiana fedha kwa Dar Express? Tunaenda mbele ama tunarudi nyuma?
Kabla hatujaenda mbali, tujiulize, je, endapo nauli za mabasi nazo zikapanda maradufu tutafanyeje? Hapo ndipo ambapo ninapingana na suala la kutafuta mbadala, badala yake tutafute jawabu.
Hata kama nauli ya kutoka uliko hadi ziliko fedha ni ndogo kuliko tozo, lakini bado njia ya kufuata na kupeleka fedha ni mbaya. Je, vipi kuhusu upotevu wa muda? Kitu ambacho kinawezeka kufanyika ndani ya sekunde mbili itabidi kigharimu siku nzima. Haijakaa sawa!
Sasa nini maana ya maendeleo ya kiteknolojia endapo mifumo ya kurahisisha maisha inabuniwa na haitumiki, kisa tu serikali imeweka mazingira magumu. Serikali itambue kuwa hii ni huduma, si anasa. Na kwa hivyo, inapaswa kuhakikisha mazingira yanakuwa rahisi ili wananchi wazifurahie huduma badala ya kukomoana kupitia huduma.
Mtukufu Rais alisema tuikosoe serikali yetu kwa staha na kupendekeza masuluhisho, lakini serikali inapaswa ianze na wao kwa kutuongoza kwa staha badala ya kutukurupua kama magari mabovu.
Nitoe wito kwa Watanzania wenzangu, tuzikate tozo hizi kwa nguvu kama vile hakuna mbadala mwingine…