Tupambane na tusikate tamaa lakini tusichoshwe na usahihi

Tupambane na tusikate tamaa lakini tusichoshwe na usahihi

Badakao

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
19
Reaction score
24
Kwa nini kuchoshwa na usahihi?

Mara nyingi kuna watu ambao huwa na msimamo wa mambo wanayoyaamini.

Mfano: Kuna binti mmoja alikuwa anasoma katika shule ya upili(secondary) na lengo lake lilikuwa ni kupata elimu bora ili awe na maisha bora na akawa akiamini kwamba endapo atasoma kwa bidii atafikia malengo yake.

Sasa siku moja kuna kijana ambaye alikuwa amefanikiwa kimaisha na alikuwa na mali nyumba na magari akamfata yule binti akamwuliza,

we binti unasoma ili upate nini? Yule binti akamjibu kuwa nataka niwe na maisha mazuri. Yule kijana akamwambia kama ni maisha mazuri mimi ninayo, akamwuliza waonaje kama ukiacha shule mimi nikuoe maana unacho kitafuta mimi ninacho.

Lilikuwa jambo gumu kwa yule binti lakini badaye yule binti akakubali kuolewa, akaamua kuachana na shule. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba yule binti hakuolewa na akawa amechoswa na usahihi.

Leo pia kuna watu ambao kwa huwa wana misimamo kwa mambo wanayoyaaminia lakini badaye hulegeza misimamo yao na kwa kufanya hivyo hujikuta wanakosa walichotegemea.

Tupambane na tusikate tamaa lakini TUSICHOSHWE NA USAHIHI.
 
Lilikuwa jambo gumu kwa yule binti lakini badaye yule binti akakubali kuolewa, akaamua kuachana na shule. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba yule binti hakuolewa na akawa amechoswa na usahihi.

Hakuolewa mara aliolewa, mbona hapa sijakuelewa.
 
Back
Top Bottom