Tupaze sauti zetu, hii sio sawa

Tupaze sauti zetu, hii sio sawa

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,200
Reaction score
12,762
Bwana Martin Niemoller {1892-1989} anasema "First they came for the socialists and l didn't speak out, because l was not a socialist then they came for the Trade unionists and l didn't speak out, because l was not a Trade unionist then they came for the Jews and l didn't speak out, because I was not a Jew then they came for me and there was no one left to speak for me".

Pale matendo yasiyo ya kiutu yanapo jitokeza katika jamii au kushamiri ni vema kuyakemea, yawe yanakugusa au hayakugusi,maana kukaa kimya ni ishara ya kuyaunga mkono.Usishindwe kuyakemea kwa sababu ya chuki binafsi,utofauti wa dini/kabila au utofauti wa itikadi ya kisiasa,maana katika udhalimu hakuna aliye salama huwa ni suala la muda tu, nawe yatakufika,kumbuka leo kwangu,kesho kwako ndivyo usemavyo msema wa wahenga.

Uzuri ni kwamba kupinga mambo yasiyo shahabiana na utu sio kosa maana huo ni wajibu wa kujenga jamii yenye utulivu,ustawi na yenye ustaarabu,jambo hili lilisisitizwa hata na Baba wa taifa Mwl.Nyerere pale alipo toa rai ya kupinga mifumo kandamizi ndani ya taifa letu.

Taifa letu kwa miongo kadhaa tulipewa sifa kende kende,kipindi cha ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika kama kisiwa cha amani {The island of peace} sasa kimegeuka kisiwa cha utekaji,utesaji na mauaji,ile sifa na taswira ya Tanzania yenye kujali utu kwa kila mmoja haipo tena,si kwa wastaafu,raia,waandishi wa habari,viongozi wa dini, viongozi wa asasi za kiraia,watumishi wa umma,vyama vya kitaaluma,wanaharakati na viongozi wa vyama vya kisiasa.

Kitu kibaya zaidi nacha kusikitisha na kinacho tia taifa hili aibu na kuliacha taifa uchi ni tuhuma za utekaji,utesaji na uuaji unahusisha moja kwa moja na vyombo vya ulinzi na usalama yaani police na usalama wa Taifa {TISS} ni mambo ya ajabu kwa vyombo hivi ambayo vipo kwa majibu wa sheria mama ya nchi {Katiba} kushutumiwa kujihusisha na kazi zilizo kinyume na majukumu yao ya kimsingi yaliyo ainishwa katika sheria.

Na hata kama tuhuma hizi niza uongo kuhusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama bado wanastahili kubeba mzigo wa lawama kwa kushindwa kutimiza majukumu yao kama ipasavyo na mwisho kuleta taharuki katika jamii.Na kama wakuu waliopo katika vyombo hivi wameshindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo wawajibike na hii haito kuwa aibu kwao bali faida kwa umma,mbona Mzee Mwinyi aliwahi wajibika na baadaye akaja kuwa Rais wa awamu ya pili,Nyinyi wa leo mnashindaje ?

Leo hii hakuna mwananchi mwenye imani na vyombo vya ulinzi na usalama ndani ya nchi hii na inachangiwa na uweledi mdogo wa baadhi ya Askari wetu wanapo timiza majukumu yao mifano iko mingi lakini hapa nitataja michache kifo cha mwandishi wa habari bwana Joseph Senga alipo kuwa akipiga picha wakati jeshi la polisi lilipokuwa likituliza ghasia,apambo mwandishi wa habari Daudi Mwangosi wa kituo cha Channel Ten, alipoteza maisha,kifo cha utata cha Stan katabalo,kupotea na kutopatikana kwa Azory Gwanda,Ben Saanane,Moses Lijeje nk kifo cha afande Tamimu {rejea kesi ya uhaini},kifo cha Akwilina Akwilini mwanafunzi wa NIT,kifo cha kijana Meshack Daudi Paka,Askari Saba wa jeshi la police kutuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara Musa Hamisi na mmoja wao kujinyonga akiwa mahabusu{Greyson Mahembe} nk.

Pia kumeibuka kundi la watu wasio julikana,ambao wanafanya matukio ya kialifu kwa watoto, viongozi wa vyama vya kiasia na wanaharakati.Watu hawa wanahusishwa na matukio mengi ya kialifu mfano ni shambulio la makamu mwenyewekiti wa CDM,Mh.Tundu Lisu,Kumteka na kumtesa msanii Roma mkatoliki,kutekwa kwa mfanyabiashara mkubwa nchini na mmiliki wa club ya Simba,bwana Mohemed Dewji alimaarufu kama Mo,kuwafuatilia wanaharakati huru na wakosoaji wa serikali hasa katika mtandao wa x mfano bwana Tito Magoti nk.

Awe uliye katika nafasi ya uongozi ndani ya taifa hili iwe kwenye chama tawala au serikalini paza sauti yako kukemea tabia hii ya kidhalimu isiyo na utu kwa taifa letu,na kama unashindwa kupaza sauti kwa kuhofia nafasi yako au kwa kuona wanaopitia magumu ni Sawa kwa sababu ni chama chenye itikadi tofauti na yako,nadiliki kusema hivi unajidanganya,ukitaka kuamini maneno yangu kwamba hakuna aliye salama katika mfumo wa kidhalimu rejea tukio la Mzee Mangula na JPM (rip) kuhusu kulishwa sumu.

Sote tunapaswa kutambua kwamba hakuna zawadi kubwa katika dunia hii kama zawadi ya uhai,hivyo kila mmoja ana haki ya kuishi,hili ndo lilimfanya hata Mwalimu Nyerere kuwaweka maadui zake wa kisiasa kizuizini wakina mzee Joseph Kasela Bantu na Christopher Kassanga Tumbo bila kumsahau mzee Abdu Jumbe na sio kuwatoa uhai wao,licha kwamba huo uwezo alikuwa nao na hakuna ambaye angemzui.

Hadithi ya mtego wa Panya iwe fundisho kwetu sote.
 
inasikitisha na inafikirisha sana..

infact,
kulikoni Taarifa officially za utekaji zinatoka HQ ya chama kwa wakati muafaka sana, at the same time pia taarifa officially za mauaji ya mateka pia zinatoka HQ ya chama kwa wakati muafaka sana, bila kuchelewa right, ?

huu ni miujiza au mpango maalumu wa hq?

hivi ni kweli hakuna taarifa za hapo katikatika kilifanyika nini, hata itolewe tu taarifa ya mwanzo wa utekaji na mwisho wa utekaji pekeyake?

anyway sawa,
huyu mtoa taarifa anakaa engo gani hasa wakati wa haya matukio ya sehemu mbili tu anazoripoti kila wakati?

hii sehemu ya katikatika kaiweka wap?🤭

R.I.P.kamanda Ally kibao
 
Sasa Kuna Citizen journalism.Pia taarifa kutoka HQ ya chama inavunja sheria gani ?
 
hakuna siala la kisheria lililovunjwa popote kwenye kutaka kujiridhisha dhidi ya utata wa kifo cha kinyama sana cha kamanda Ally Kibao...

hakuna haja ya kwa yeyote kutishika , hakuna haja ya ukali wala kibabaika katika kuhakikisha haki na stahiki za kamabda Ally Kibao zinapatikana na wahusika wanawajibishwa ipasavyo kulingana na sheria :pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom