Tupeane Elimu: Fahamu tofauti kati ya Toyota Wish na Toyota Isis

Tupeane Elimu: Fahamu tofauti kati ya Toyota Wish na Toyota Isis

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
Kuna sehemu tumeulizwa kuhusu tofauti ya Toyota Wish na Toyota Isis. Tumempatia majibu yafuatayo.

Hizi gari mbili ni ngumu sana kuzitofautisha kitaalamu kwa sababu injini na gia box zinafanana. Itafaa mchaguaji wa gari hizi aangalie zaidi anapendelea gari ipi zaidi kati ya hizi mbili kwa kuzitazama machoni.

Zote mbili zina injini aina ya 1ZZ ya Cc 1800 ambayo ni viti yenye sifa ya matumizi madogo zaidi ya mafuta. Pia zote zina injini ya 1AZ ya Cc 2000 ambayo matumizi yake kwenye mafuta ni juu kidogo. Ila pia hii injini ya pili haishauriwi sana kwa kua hutumia umeme mwingi zaidi jambo ambalo linaifanya iwe na complications pindi inaposumbua.

Wish imewekewa siti 7 kama ilivyo kwa Isis ingawa uzuri wa Wish ni kwamba ukilaza hizo siti za nyuma nafasi ya buti inakua kubwa zaidi kuliko ilivyo kwa Isis.

Pia kuwa suala ya uzito wa gari. Wish kwa wastani ina kilo 1360 na hivyo kuifanya iwe nyepesi barabarani na yenye matumizi madogo zaidi ya mafuta haswa kwa safari za mjini kwa kuwa kwenye safari ndefu balance yake huwa ndogo sababu ya wepesi ukilinganisha na Isis yenye Kg 1470 ambayo kwenye mafuta yaweza kutumia juu kidogo ya Wish lakini huwa ni nzuri zaidi kwa safari ndefu sababu uzito wake huifanya iwe imara kulinganisha na Wish.

Wish ina viegemeo vya dereva na abiria wake kwa mbele wakati Isis inacho cha upande mmoja tu wa dereva.

Lakini pia Wish ina milango inayofunguka kawaida kama ilivyo kwa magari mengi, wakati Milango ya Isis ya nyuma ni ya kuslide ambapo kama matumizi ni ya fujo kuna uwezekano wa kung'oa vitasa hivyo au kuharibu bearing zake mara kwa mara.

Kwenye gharama ya manunuzi kwa kuagiza Wish iko juu na huanzia 12m wakati Isis huanzia 10,600,000.


BG680696_3f1488.JPG
BG695223_1f45c2.JPG
 
Back
Top Bottom