bilemasome
Member
- Oct 31, 2016
- 48
- 9
Habari Ndugu, jamaa na marafiki
Sisi sote tumesikia au tumepitia kuhusu kutapeliwa kwenye ununuzi wa viwanja.
Hii hali inachosha na inaumiza sana, hasa kwa yule aliyetapeliwa kwenye ununuzi wa viwanja.
Wengi wetu huwa tunawacheka waliotapeliwa au kununua kiwanja chenye mgogoro (nakuombea usipitie katika hii hali-inaumiza sana).
Hii ni kutokana na watu kukosa elimu juu ya ununuzi wa kiwanja.
Binafsi nimejaribu kutafuta hii elimu walau inisaidie kujua ABCs za kufuata ili niweze kuepuka hizi changamoto (kutapeliwa/kununua kiwanja chenye migogoro) nimekosa, yaani sijaona mtu ameliongelea hili.
Siku hizi kumezuka kampuni mbalimbali zinauza viwanja- yaani wanakuuzia kwa mita za mraba n.k - jinsi ya kuwajua kama ni kampuni yao ni halali au laa unajuaje?
Au ni taratibu zipi mtu afuate, endapo atanunua kiwanja kutoka kwa mtu.
Tena hapa unakuta umepelekwa na dalali kwa huyo mtu. Ni taratibu zipi mtu anabidi afuate.
Ombi Langu:
Najua wadau na wanasheria wa haya mabo ya viwanja mpo wengi humu, ninawaomba, Mtupatie elimu kuhusu ununuzi wa viwanja na mambo ya kuyaepuka ili tuweze kuzikabili hizi changamoto za kutapeliwa na ununuzi wa viwanja vyenye migogoro"
Mchango wako katika hili, utatusaidia Watanzania wengi, nami naahidi elimu nitakayoipata hapa nitaihubiri na kuisambaza kwa watu wote wenye kiu ya ununuzi wa viwanja.
Natanguliza Shukrani
Mungu akubariki wewe utakayeweka mchango wako wa elimu hapa!