Nilifanya kwa muda nikaacha kwa changamoto ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu,
Lakini changamoto nilizokuwa nakutana nazo ni polisi pale nimeuziwa vyuma vya wizi,
Mwanzo nilinunua mzani ambao una label ya WMA(unatambulika na wakala wa vipimo Tanzania) sababu ukikutwa na mzani ambao hautambuliki ni makosa, nikawa nanunua kwa kilo sh 550 namimi naenda kuuza NYAKATO STEEL KWA 1,000 kwa kilo, na kuna vyuma vizito ambavyo nilikuwa siuziwi kwa kilo bali tuna-bargain ,kuanzia plate, Angle Iron za milimita tatu na kuendelea.
Ishu nyingine inakuja kwenye mtaji, maana unaweza letewa vyuma ambavyo huwezi kufika bei (hii ni kwenye bargaining) sio vya kupima.
Obvious ni biashara nzuri, ila unatakiwa uwe na kibali ili uifanye bila usumbufu na usinunue nyara za serikali(mifuniko ya chemba za barabarani,vyuma vya Tanesco na vinginevyo)