Tupeane mbinu za kuacha uvutaji sigara

Tupeane mbinu za kuacha uvutaji sigara

Meneja CoLtd

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
122
Reaction score
143
Naanza kutanguliza salamu na shukurani hapa JF. Pili nawasilisha hii mada kwenu wajuzi tusaidiane ni mbinu zipi mtu anaweza kuzitumia kupunguza na kuacha kabisa kuvuta sigara

1f7070f18c7f805711aab8e96ae41cc4.png

Baadhi ya mbinu ambazo zimesikita zikitumiwa na watu kuacha kuvuta sigara ni;

1 Kupunguza idadi ya uvutaji wa sigara, hapa kama mtu alikua anavuta sigara 10 basi apunguzu idadi kidogokidogo mpaka sigara 2 au 1

2 Kutafuta kilevi mbadala ambacho hakina madhara mfano PIPI KALI, mvutaji sigara anapohisi alosto anapaswa atumie pipi kali kama mbadala wa uvutaji sigara

3 Kujiweka bize na shughuri za utafutaji pesa, maendeleo na kujichanganya na watu wa imani (makundi ya dini) maana kwa kiasi kikubwa ushawishi wa kuvuta sigara unakuja ukiwa pekeyako au ukiwa na kundi la wavuta sigara.

4 Mwisho kabisa uvutaji wa sigara utaachwa endapo mvutaji ataamua na kujifosi mwenyewe kuacha kuvuta sigara na KUYAJUA MADHARA ATAKAYOYAPATA KUTOKANA NA UVUTAJI WA SIGARA.

Pia soma
- Dawa ya kuacha sigara
 
Aisee poleni wavutaji, kuna jamaa yangu nae huo ulevi unamtesa sana.
Midomo yake imeshaanza kua na weusi.

Bei rahisi ya sigara inafanya wavutaji wasiache.
 
Back
Top Bottom