Tupeane Updates: Hali ya mtandao ikoje mahali ulipo? Shughuli zako zinaenda kama kawaida?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Hali ya mtandao imekuwa ya kususua tunaenda karibia wiki ya tatu sasa. Ni shida kuingia katika baadhi ya sites kiasi kwamba inabidi utumie vipi.

Pia soma: Historia ni mwalimu mzuri, msiseme sikuwaambia!

Wale ambao kazi zetu zinategemea uwepo wa mtandao kwa sehemu kubwa zinaathirika vibaya, lakini hata kama shughuli zako hazihusishi mambo ya mtandao kwa kiasi kikubwa bado utapata athari hizi hasa upande wa mawasiliano na kupata taarifa.

Pia soma: Shida ya mtandao inayoendelea nchini tatizo ni nini? Serikali mpo kimya kampuni za mitandao mpo kimya! Sasa nani ana majibu?

Tupeane updates za hali ya mtandao sehemu tulipo huenda itasaidia kupata namna na kuepuka adha hizi na wale wataalamu wa VPN washauri VPN nzuri za kutumia ili michakato iende.
 
Hii kitu imenipa stress sana juzi, nilijibana nikamuagiza mshikaji wangu Pixel unlocked US version, amefika juzi najaribu kuingia hapa na pale internet hakuna, aisee nilipatwa na mshituko nikajua tayari imekula kwangu.
 
mimi sijaexperience tatizo hili labda kidogo siku ile mtandao wa tigo ulipozingua lakini napo haikuwa tatizo kubwa sana ilikuwa kidogo unashuka kwa dakika kadhaa then unarudi sawa ila toka siku hiyo niko sawa kabisa.
 
Yaani ni balaa, yaani kama saivi vitu vinachukua muda kweli kuload, imebidi niwashe VPN
 
mimi sijaexperience tatizo hili labda kidogo siku ile mtandao wa tigo ulipozingua lakini napo haikuwa tatizo kubwa sana ilikuwa kidogo unashuka kwa dakika kadhaa then unarudi sawa ila toka siku hiyo niko sawa kabisa.
Hongera yako, mimi mpaka sasa napitia changamoto hiyo, jana ilikuwa mbaya sana
 
Airtel ndio kidogo wapo vizuri lakini tigo na voda ni hovyo kabisa.
 
Mtandao unasumbua ila ukiwasha VPN unakubali? Something doesn't add up.
 
Wakuu,

Hali ya mtandao imekuwa ya kususua tunaenda karibia wiki ya tatu sasa. Ni shida kuingia katika baadhi ya sites kiasi kwamba inabidi utumie vipi.

Pia soma: Historia ni mwalimu mzuri, msiseme sikuwaambia!

Wale ambao kazi zetu zinategemea uwepo wa mtandao kwa sehemu kubwa zinaathirika vibaya, lakini hata kama shughuli zako hazihusishi mambo ya mtandao kwa kiasi kikubwa bado utapata athari hizi hasa upande wa mawasiliano na kupata taarifa.

Pia soma: Shida ya mtandao inayoendelea nchini tatizo ni nini? Serikali mpo kimya kampuni za mitandao mpo kimya! Sasa nani ana majibu?

Tupeane updates za hali ya mtandao sehemu tulipo huenda itasaidia kupata namna na kuepuka adha hizi na wale wataalamu wa VPN washauri VPN nzuri za kutumia ili michakato iende.
TIGO NI SHIDA
 
Hivi VPN si tulikatazwa kuipakua bila kibali wakuu?
Nje ya mada wasiojulikana tunawafanyaje Sasa wakuu?
 
Back
Top Bottom