Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Biashara ya bodaboda na suzuki cary kwa kusubiria hela ya wiki...

Bodaboda zilikiwa tano, kila moja ilikuwa inaleta 50,000/- kwa wiki. Hela ya service ilitoka hapo hapo, wastani wa 8,000/- kwa wiki EXCLUDING major breakdown.

Sasa uswahili wa madereva mara mtu alete 30,000/- na maelezo ya 20,000/-.... kingine wizi... baadhi ziliibiwa ila kwa vile niliziwekea bima kubwa nikalipwa na bima. Mwishi niliziuza zote zilizobaki

Suzuki cary nazo mbwembwe na longo longo za madereva zilokuwa ishu. Unfortunately moja iliibiwa baada ya dereva kuuwawa. Bima kubwa ilinisaidia kulipwa.

Risk ni nyingi. Hivyo vi-cary hubebeshwa mizigo kuliko uwezo wake.
Matrafiki nao barabarani wakiona cary ni kama wanaona hela inayotembea... hawavichi vikafanya kazi zake kwa uhuru.. kilichobaki nikakiuzilia mbali

By the way, kwa mtu anayetaka kufanya biashara ya bodaboda, ni bora afanye kwa mkataba. Unanunua bodaboda 2M, unachukua 10,000/- kila siku kwa miezi kumi au zaidi kutegemeana na makubaliano mnayoandikishana. Muda ukifika inakuwa ya uliyeandikishana naye
 
Ngalikihinja,
Ila Suzuki carry vinaonewa sana.
Mwaka flani nikiwa Dar jamaa yangu flani alikuwa anakimiliki na kuendesha mwenyewe ila kashkash za trafiki zilikuwa kubwa sana
 
mi ni biashara ya kuuza nguo za mtumba mnadani, aise yan baro la jeans unanunua laki sita, kilo mia lkn jeans unazozkuta ndani ni kichekesho ilinikata mtaji nikaamua nilime nyanya tu. na ctaman tena mambo za mtumba hela yake n ya moto ata yamoto band haifkii.
 
*OFFICE/KIGOLI INAUZWA WAPENDWA IPO MTAA WA MAFIA NA SKUKUU NI KIGOLI CHA PEMPARS NA VITU VYA WATOTO INAUZWA NA KILA KITU KILICHOMO MWENYEWE KAHAMISHWA KIKAZI HIVYO WANAHAMA NDO AKAAMUA AUZE KWA MAELEZO ZAIDI 0688008799 NO YA MUHUSIKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu biashara ya Mpesa inachangamoto nyingi sana ila hii ya kupoteza pesa ni jambo la kawaida mno. Nimeifanya kwa muda mrefu sana. Unafunga hesabu jioni kukuta laki 3 hakuna ni jambo la kawaida mno. Unameza mate machungu unasubiri commission ije kufidia hasara.
 
Mkuu kwenye biashara ya mpesa,Tigo pesa lazima utapigwa tu Nina uzoefu na hiyo biashara 6 yrs now so I am talking from my experience sio chanjanja Wa kijiweni tu mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu....hesabu ya Suzuki Carry kwa wiki ilikua bei gani
Nilikuwa naletewa 125,000/- kwa wiki...
Mwanzo biashara ilikuwa nzuri sana... maana
50,000 X 5 = 250,000/- bodaboda

125,000 X 2 = 250,000/- carry

Total 500,000/- kwa wiki, then utoe service cost
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…