Tupeane uzoefu: Ni namna gani nzuri ya kuwaenzi wapendwa wetu waliotangulia mbele ya haki?

Tupeane uzoefu: Ni namna gani nzuri ya kuwaenzi wapendwa wetu waliotangulia mbele ya haki?

Baba Mama

Senior Member
Joined
Apr 1, 2018
Posts
107
Reaction score
138
Utukufu kwa Mungu, wa uzima na wokofu!

Wapendwa wana jamii.

Maisha yana michakato mingi sana. Na ndani ya maisha kuna wapendwa wetu kwa namna moja ama nyingine huwa ni nguzo kuu ya kutusaidia kujenga maisha yaliyo bora kwa vizazi hadi vizazi.

Kwa bahati mbaya sana, ama kwa makusudi ya Mungu wa uzima na wokofu wapendwa hawa hututoka machoni petu, hutangulia mbele ya haki.

Sasa, ni heshima na utukufu kwa Mungu kuwaenzi watu hawa, maana kupitia kwao ndipo milango ya ufahamu kuhusu Ulimwengu zilifunguliwa.

Ni vema pia, kukumbuka kuwa safari yetu ni moja. Tunazaliwa na tunakufa kwa wakati Mungu Muumba aliokusudia.

Naomba tupeane ushauri wa hapa na pale, Je, ni namna gani bora ama ifaayo kuwaenzi wapendwa wetu hawa?

Kipekee, naomba kumualika Mshana Jr
 
Anzisha taasisi ya ngos kwa ajili ya kusaidia jamii...
Mfn MARIA FOUNDATION.... Toa misaada kwa kutumia jina la hiyo taasisi..... Jenga kiuto cha watoto yatima....somesha yatima.....
Hakika utamuenzi mpendwa wako mpk dahari....
Mfn nobel prize.......
MWANZILISHI wake ameendelea kuishi nasi kupitia hizo tuzo
 
Kufanya mambo mema yote waliokuwa wakiyafanya some time tulia kimya peke yako fikiria jinsi ulivyokuwa ukikaa nao/ ukiishi nae marehemu..mabaya yake mwachie mwenyewe mema yake yachukue.
 
Utukufu kwa Mungu, wa uzima na wokofu!

Wapendwa wana jamii.

Maisha yana michakato mingi sana. Na ndani ya maisha kuna wapendwa wetu kwa namna moja ama nyingine huwa ni nguzo kuu ya kutusaidia kujenga maisha yaliyo bora kwa vizazi hadi vizazi.

Kwa bahati mbaya sana, ama kwa makusudi ya Mungu wa uzima na wokofu wapendwa hawa hututoka machoni petu, hutangulia mbele ya haki.

Sasa, ni heshima na utukufu kwa Mungu kuwaenzi watu hawa, maana kupitia kwao ndipo milango ya ufahamu kuhusu Ulimwengu zilifunguliwa.

Ni vema pia, kukumbuka kuwa safari yetu ni moja. Tunazaliwa na tunakufa kwa wakati Mungu Muumba aliokusudia.

Naomba tupeane ushauri wa hapa na pale, Je, ni namna gani bora ama ifaayo kuwaenzi wapendwa wetu hawa?

Kipekee, naomba kumualika Mshana Jr

1. Wakumbuke kwa matendo yao mema, usiwaabudu ila mwabudu Mungu
2. Tenda mema kwa watu wote ikiwezekana katika kiwango ambacho ni zaidi ya kile kilichowahi kufikiwa na wale wote unaowajua, waliotangulia mbele ya haki
 
Michango mizuri sana.....tuendelee wakuu !
 
Back
Top Bottom