Moto wa volcano
JF-Expert Member
- Jun 3, 2018
- 1,148
- 2,815
Kuna kipindi niliwahi kuwa na biashara nzuri na wafanyakazi pamoja na usafiri wa kutembelea ulionipa heshima kila niendapo, ikatokea biashara ikayumba mambo yangu yakaharibika ikapelekea kuangukia kwenye madeni mpaka kuuza gari langu aisee heshima yangu ilishuka mpaka sakafuni kuna marafiki waliacha kunipigia simu wengine wakaanza kunichukulia poa.
Kupitia Mapito hayo nikajifunza mengi kuhusu walimwengu, nikarudi mzigoni kazi kazi kwa bidii mambo yakaanza kurudi kwenye mstari nikafungua biashara mpya na nikapata usafiri mpya .walioacha kupokea simu zangu kwa dharau wamebaki na aibu . Sasahivi sicheki na makima nakula good time zangu kivyangu . Kuteleza sio kuanguka ukiwa imara unaweza kusimama tena