Tupendekeze dar iwe center ya Japanese used car kwa nchi za zote Africa especially landlocked

Tupendekeze dar iwe center ya Japanese used car kwa nchi za zote Africa especially landlocked

wakomong'we

Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
30
Reaction score
2
Ndugu wana Board habarini za weekend,Leo nimekuja na pendekezo moja kwamba ni kwa nini serikali yetu isijipange kuwashawishi wajapan na serikali yao kuweka soko la magari yao used hapa Dar,kutokana kwamba nchi nyingi za Africa zinanunua haya magari kwa wingi sana,hoja yangu hapa ni kuifanya Dar iwe kama kitovu cha kuuzia haya magari kwa nchi zote au zilizo nyingi barani Africa.Ambapo kupitia hili serikali itakusanya kodi zaidi na zaidi na kuzifanya bandari zetu kuwa more competitive.Huu ni mtazamo wangu sijui nyie wadau mnaonaje.ASANTENI SANA.
 
Mawazo gani haya sasa? wewe huna habari baadhi a Nchi za Africa, magari used hayaruhusiwi? kwa hiyo unataka Tanzania iwe Dampo la magari kutoka Japan? Nchi kama South, Nigeria na zinginezo wao magari used si dhani kama uanaruhusiwa,

Wewe badala ya kusema wajenge kiwanda cha Kuunganisha Vipuri wewe unagubiri Duka la kuyauzia, Ingawa hata kwa Kiwanda ni ngumu sana kwa sababu tiyali Toyota, Nisan, Tdi, na makampuni mengine wana viwanda vyao south Africa,
 
wajapan wanajenga Kenya kiwanda cha ku-assemble Magari aina ya Hino .... buses and trucks
 
wajapan wanajenga Kenya kiwanda cha ku-assemble Magari aina ya Hino .... buses and trucks

Hivi huko Kena si ndo hata kuna ofisi za Nokia? Na Tecno kwa Nchi za Africa wana Ofisi Kenya na Nigeria pekee, Tatizo huku Tanzania hakuna anaye jari kila mtu anaangalia Tumbo lake na famailia yake, that is why wanakimbilia kenya, huku

Nashangaaga sana hata Ofisi za Magic Swahili eti ziko Kenya na watangazaji wote ni wa Kenya, hapo ndi huwa nachoka, Watanzania kwa kifupi tumelala usingizi wa Pono halafu tunajifana tunajua sana kumbe hakuna kitu
 
kwa bandari yetu ilivyo kwa sasa.
Hii ita waletea shida sana.
 
Ufanisi wa bandari yetu na foleni za kufa mtu hatutaweza hilo..

Hivi sasa tu bandari haipo busy lakini kila siku fujo na vurugu watu kuibiwa vitu,, meli zinapangishwa foleni za kipumbavu na ufisadi halafu unataka tuwe Hub ya magari ya kijapan si itakuwa balaaa
 
Hali ya hewa tu hairuhusu, chumvi too much gari hazidumu zitapata kutu zoote ndan ya mda mfupi.
 
hapana kuwa dampo, ila vzr kuwa manufacturer hata nguo bora za kichina than kuwa middlemen ya used cars
 
Ndio hata dubai wanavyofanya ile ni soko kuu la magari used ya japan..faida zake ni kubwa sana hot. Zao zinajaa pindi watu wanapokuja kufanya shopping..ndege zao emirates na etihad zinajaza wanunuzi wanaokuja fanya shopping ndio maana airlines zao zinakua kila siku..dubai haina mafuta kama wengi wanavyofikiri ni akili tu...leo hii tungetumia bandari zetu vizuri na tax ikawa chini wale waafrika wanaokwenda dubai wote wangekuja bongo....00971504374386
 
Back
Top Bottom