Tupeni historia ya Mbuyu wa pale kona ya kwenda Masaki, Kwanini haukatwi?

Tupeni historia ya Mbuyu wa pale kona ya kwenda Masaki, Kwanini haukatwi?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Hivi nani anaijua Historia haswa ya ule Mbuyu wa pale ‘Mbuyuni’ kona ya kwenda Oysterbay/Masaki.

Maana inashangaza vile umekaa katikati ya Barabara na haujawahi kukatwa!!

Sahizi mwendokasi nao wanaukwepa kuukata sasa sijui watapitisha wapi Barabara yao?
 
Pale ulipo ni mazingira mazuri tuu mkuu si kila kitu ni cha kuondoa huenda umeachwa ili kuweka upekee wa hiyo barabara
Walishindwa kuukata enzi hizo, wakaamua kuuacha!

Msasani Club pale wanaweza kukupa visanga kamili walipokuwa wanafanya ujenzi eneo lile, pengine hata balozi ya usa pale!

Sio suala la mazingira au mandhari, ingekuwa hivyo si ingepishwa miti mingi tu!
 
Hauzuii chochote! Kwanza unaleta mandhari nzuri.

Na kingine ni sehemu ya historia/kumbukumbu kwa sisi wengine ukuaji wetu.
Jibu zuri 👍🏾, bhasi haustahili kukatwa kama umebeba historia fulani nzuri.
 
Hivi nani anaijua Historia haswa ya ule Mbuyu wa pale ‘Mbuyuni’ kona ya kwenda Oysterbay/Masaki.

Maana inashangaza vile umekaa katikati ya Barabara na haujawahi kukatwa!!

Sahizi mwendokasi nao wanaukwepa kuukata sasa sijui watapitisha wapi Barabara yao?
Kwanini ukatwe?
 
miti mikubwa kama hiyo mfano miembe,mkorosho na mbuyu inayobeba majina ya eneo ukisikia panaitwa labda mkoroshini,mwembeni au mbuyuni hizo sio sehemu za kawaida kuwa ni vilinge vikubwa sana vya wale wa upande wa giza pia ni madhabau za kuzimu..ndiomaana wachina wakiwa wanajenga barabara na wakataka kukata huo mbuyuni au mwembeni kabla ya kukata lazima wafanye kafara kubwa au zindiko kubwa ndio waukate ila wakiona ni pazito wanapaacha kama kulivyo maana ni hatari..haya mambo yapo kiroho zaidi sio rahisi kuelewa kwa akili na macho ya kawaida..nyie endeleeni kusema tu ni kivutio cha utalii sijui kupendezesha mazingira hayo mengine yapo nje ya upeo wetu.!
 
Pale nasikia wazaramo walikuwa wanakutana kucheza Ngoma enzi za Mjerumani
 
Kipindi niko Primary na washkaji zangu asubuhi tukamkuta jogoo,nazi zimepasuliwa,umemwagwa mchele nk nk..Kuna mwenzetu mmoja akasema msinichezee akachukua jogoo akazoa na mchele tukaenda kula gheto..kiufupi nimeshafaidika na huo mbuyu usikatwe😂
 
Back
Top Bottom