pipi mti
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 764
- 514
Wakuu Kama topic inavyojieleza hapo juu. Kumekuwa na Hali ya mtu kutumia avatar ya mtu mwingine kitu ambacho sio kizuri. Kuna watu ambao ni maarufu duniani kama Barack Obama, cr7, messy na wengine wengi na hapa nchini kama Tundulisu, Magu,samatta, Lowassa na wengine wengi. Si vibaya kuweka picha ya mtu unayempenda kama avatar yako, lakini tatizo linakuja pale mtu anapoichukua picha ile ile ambayo mwingine anayoitumia wakati watu hao ukiingia mtandaoni wanapicha nyingi tofauti na unaweza Ku download na kuzifanya kuwa avatar yako.Pia kwa avatar za cartoon inatokea Mara nyingi.
Wapo wanaoiba avatar makusudi na wapo ambao wanajiunga na kuchagua avatar izo kwa kutofahamu kwamba kuna wenzao wenyeji wa humu wamekua wakizitumia tangu miaka ya nyuma. Binafsi nilipojiunga nilianza kwa kutumia avatar hii.
Baadaye nikagundua kwamba kuna waliotangulia kabla yangu wamekua wakiitumia tangu muda na wengine wageni walionikuta wameanza kuitumia ivyo nikaona ni busara kuwa na avatar nyingine ambayo ni hii
Lengo likiwa ni kuwa na avatar ya peke yangu.
Tupia avatar yako hapa ili kuthibisha wewe ndio mmiliki halali wa avatar iyo humu Jf na kuwasaidia wanaJf wapya kuepukana na avatar ambazo tayari zinamilikiwa.