Baada ya solomoni kufariki,mtoto wake rehobam akatawazwa kuwa mfalme,
waisrael ambao walikuwa wamechoshwa na utawala wa mabavu wa solomoni na kodi za kila aina,wakawatuma watu wakamwambie mfalme mpya alegeze kidogo watu wanalalamika asiwe kama babake.
Mfalme mpya kusikia hivyo,akaenda kuomba ushauri kwa viongozi waliokuwa wa umri mkubwa ambao aliwakuta serikalini,wakamwambie wasikize watu wako uwalegezee japo kidogo nawe utatawala vizuri tu.
Mfalme mpya baada ya hapo kawafuata washauri wake wapya wale alioingia nao serikalini,
ambao wengi walikuwa vijana vijana tu wa rika kama la yule mungu wa kariakor.
Wakamshauri na kumwambia wewe wakazie tu bamba to bamba,
mfalme karudi kwa wazee wa kiisrael akawambie.,"mwende muwambie wananchi aliyokuwa akiwafanyia babangu solomoni ,mimi nitawafanyia mara tano zaidi.
Wazee wa kiisrael wakapeleka message kwa watu wao.
Kilichotokea waisrael wakajitenga,makabila 10 yakajichagulia mfalme wao na kuanzisha ufalme wa israel,
wakimuacha mfalme mwana wa solomoni na makabila mawili ambayo yakaunda utawala wa yuda,na hizo nchi mbili ziliishi kwa uhasama na vita mpaka dakika ya mwisho .
Haya maandiko yako ndani ya bibilia sikumbuki kitabu kipi