Ukivaa kiatu kimoja mama yako atakatika ziwa moja
Ukigeuza kiatu juu chini unamtukana Mungu
Mtoto akitia ufunguo mdomoni haoti meno
Mtoto akinyonyeshwa titi na mwanamke ambae hatoi maziwa atakuwa bubu
Mjamzito akikalia kinu atazaa mtoto miguu itatangulia
Mama mwenye uchungu akiwa kafunga kilemba cha juchwa (scarf) hawezi kuzaa ng'oo mana anakuwa kama kajiwekea kitanzi
Usiite mtu usiku kwani shetani atalijua jina lake then atakuja na yeye kumwita na akimchukua harudi tena
Mtoto mchanga kuwekewa ndimu, kisu na kaa la kupikia ili iwe kinga
Ukizika kitovu cha mtoto chini ya mnazi atakua mrefu
Mtoto akicheka wakati amelala anakua anaambiwa na malaika kuwa baba yake atakufa so anafurahia urithi.
Na akilia anaambiwa na malaika mama yake atakufa, so analia atakosa Nyoyo.