TUPIA UONGO WOWOTE AMBAO ULIDANGANYWA NA MZAZI WAKO ILI KUKUJENGA KIAKILI

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Salam salaam!!! I hope yu wazima wa afya tena bukheri kabisa, nimejikuta nikiwa nacheka peke yangu baada ya kukumbuka UONGO au Stories nilizokua nadanganywa na baba ili anijenge kijana wake kifkra na kujiamini.

Huu Ni Uzi maalum nimeuanzisha kila mmoja watu apite na ata changia
UONGO alioambiwa na wazee wake kipindi yupo mtoto.

Mimi naanza na hivi.

Baba aliniambia kipindi yupo kijijini akiwa anachunga ng'ombe katika wale ng'ombe kuna mmoja alipatwa na uchizi akaanza kuleta vurugu pale kijijini maana Kijiji akikua mbali na mahali alipo kuwa anachungia.

"Yule ng'ombe alifanya vurugu watu wote wakakimbilia Ndani, basi mwanangu Mimi nikaona hii haiwezekani "

"Nilichukua rungu nikamfata Yule ng'ombe na yeye aliponiona akaanza kuja Kwa spidi kunifuata Mimi wanakijiji walikua wanachungulia dirishani na wengine wakawa wanasema nikimbie , Yule ng'ombe alikuja nikajifanya Kama nakimbia huku Ana nifuata nika piga Kona ya gafla ng'ombe alipitiliza basi pale pale nikampiga rungu Moja tu la kichwa Yule ng'ombe hakuinuka tena .[emoji63][emoji63]

Halafu akamalizia "wanakijiji walinisifu sana wakasema Mimi ndo mwanaume'"

(2) "darasani nilikua nashika namba Moja au mbili yaani nikifeli sana Ni namba tatu"
Ana malizia Kwa kusema "wewe utakua umerithi Kwa mama yako huko ndio hawana akili"

(3) Mimi wasichana walikua hawanisumbui maana Mimi nilikua mjanja sana unajua Kwa nini,??

"Yaani nilikua nikipata mmoja tu hiyo siku ya kwenda kufanya mambo yetu nilikua najifunga kamba kiuoni naivalisha na Pete basi unakuta nikivua nguo zangu zote msichana anaanza kunishangaa akitoka hapo Ni lazima akawahadithie wenzie na wenzake nao wakisikia hivyo lazima wanitafte ili waone maajabu yangu ya
Kamba nilio ivalisha pete hapo ndio na yeye namaliza kazi "[emoji23][emoji23][emoji23]

Huwa nacheka sana nikikumbuka saundi za Mzee.

DONDOSHA SAUNDI ZA WAZEE TUCHEKE HAPAAAAA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mods naomba huu Uzi upelekwe kwenye jukwaa husika hapa siyo mahala pake samanini Kwa usumbufu.
 
Duuuu!

Vipi hiyo mbinu ya kuweka kamba kiunoni unaifunga na Pete bado unafanya hivyo hadi zama hizi?!
 

Mungu wangu, sema kwa kuwa sio kweli!! Baba anaweza kumsimulia mwanae jambo hilo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…