D TARGET
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 223
- 98
Kuna binti nilikuwa ninamahusiano naye ya kimapenzi, Binti anaishi mkoa wa Dodoma mi ninaishi Pwani, huyu binti kunakipindi aliniambia anaujauzito wangu, hyo ilikuwa ni baada ya mimi kwenda Dodoma na kushirikiana naye kimwili, then mi nikarudi Pwani, Baada ya kunipa taharifa, muda ulivyokuwa unazidi kuendelea ikawa tunaendelea kuwasiliana na anapoitaji matumizi nikawa namtumia kama kawaida.
Ilivyofika miezi Tisa Binti akajifungua mtoto wa Kiume! Baada ya binti kujifungua akaja Mpk kwangu then nikampeleka mpk Iringa kwa wazazi wangu, ili wapate nafasi ya kumpa pongezi zao, na kumfahamu mjukuu wao. Baada ya binti kukaa kwa wazazi kama wiki tatu hv, zikatokea rumous kuwa binti anatembea na Moja ya wapangaji wa pale nyumbani kwa wazazi wangu, binti nilivyomuuliza akabisha kwamba hakuna kitu kama hcho. Siku chache zilizofuata binti akaondoka Nyumbani na kurudi Dodoma, akada mmiliki wa nyumba aliyopangisha uko Dodoma amempigia simu na kumwambia kuwa anataka kodi ya nyumba yake lasivyo atatoa vyombo vyake nje hvyo ameamua kwenda ili akamalizane na Baba mwenye nyumba.
Ikawa tunaendelea kuwasiliana na kusaidiana kama kawaida ktk kipind chote, na akawa amedai kuwa muda siyo mrefu atarudi kumleta mtoto kwangu kwani baba mwenye nyumba wamesha malizana.
Hv majuzi nimempigia simu nikashangaa simu yake imepokelewa na mwanaume, jamaa akajitambulisha kama yeye ni Mume wa huyo Binti, aikuwa shida nikamwambia mi ni mzazi mwenzake na huyo binti! Jamaa akiniambia ok we ndiyo Baba Akram, ikabidi nigune kidogo, nikamwambia mi siyo baba akram mi Baba Junior! Jamaa akaniuliza Junior ndio nani, sababu jamaa alikuwa mwelewa ikabidi tuanze kujuzana zaidi, mwisho wa siku nikagundua kuwa kumbe kuna Jamaa mwingine ambaya naye pia ni Baba wa Yule Mtoto na ndiye aliyempa yule mtoto ilo jina la Junior, na huyo jamaa ndiye anayeishi na yule mtoto kwa sasa baada ya yeye Binti kupewa ujauzito na huyo jamaa anayeishi naye kwasasa.
Binti nikimpigia simu anabaki anajing'ata ng'ata tu, sasa wadau wa JF haswa wale ambao wanaijua vizuri sheria ya mambo ya uzazi, nimfanyieje huyu binti?