Tupo kwenye zama ambazo mtu mwenye kisu kikali ndio mla nyama

Tupo kwenye zama ambazo mtu mwenye kisu kikali ndio mla nyama

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
ZAMA ZIKIBADILIKA NAWE JIFUNZE ZISIKUTOE KWENYE MFUMO.

Kuna zama ajira zilikuwa nje nje ila sasa ni lazima ufanye usaili na tena ufaulu huo usaili.

Kuna zama fursa zilikuwa zinatafuta watu ila sasa bila kutumia nguvu hizo fursa utaishia kuzisikia tu hewani.

Kuna zama mpaka wenye ufaulu wa daraja la tatu walipata vyuo tena kozi za afya lakini sasa mpaka daraja la pili wanakosa vyuo , ushindani upo juu.

TUPO ZAMA AMBAZO MWENYE KISU KIKALI NDIO HULA NYAMA.

Hizi zama zinataka uvuje jasho sana tena kwa ubunifu wa hali ya juu ili uweze kuchaguliwa na mfumo la sivyo utaishia kulalamika tu huku wengi wakinufaika.
#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako.
 
Back
Top Bottom