GARETHBALE
Member
- Dec 22, 2013
- 76
- 333
TUHARAKISHE KUWACHANGIA CHADEMA ILI TURUDI KWENYE SUALA LA SUMU NDANI YA MWILI WA MZEE MANGULA.
Taarifa ya Kamanda Mambosasa bado inakera kwenye vichwa vya wengi! Tunataka taarifa ya Madaktari wa Muhimbili.
Tunataka wale wote waliokuwa na Mzee Mangula wakati anatoka jasho na kudondoka waandike maelezo kwa sababu hao kwa vyovyote vile ndiyo watuhumiwa namba moja.
Haiingii akilini eti watu hao waachwe huru halafu Polisi waanze kutafuta watuhumiwa nje ya jengo la CCM Lumumba. Waliopo nje ya Jengo la Lumumba ni Wapinzani.
Kama alianguka mara baada ya kikao na ikabainika kuwa alilishwa sumu, kwa akili ya kawaida, Wabaya wa Mzee Mangula walikuwa ndani ya jengo la Lumumba.
Polisi mnashindwa nini kuwahoji wajumbe wote wa Kamati Kuu ili mhusika ajulikane? Aidha watu tunataka kujua hali ya mgonjwa na aina ya sumu aliyopewa.
Na taarifa hiyo itolewe na Madaktari bingwa wanaomtibu! Tumepata habari kuwa Ikulu imekataza watu wasiende kumjulia hali kule alikolazwa. Kwanini? Ikulu inaogopa nini watu wakienda kumwangalia?
Hakika mwaka huu una mengi ya kuchekesha na mengi ya aibu. Tuombe afya, tuone mengi!