Turudi tena Eden kidogo.

Turudi tena Eden kidogo.

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Posts
1,585
Reaction score
1,546
Heshima kwenu nyote Wana Jamii Inteligence.
Nimepitia uzi wa mwanajamii Mwenzetu (heshima kwake) unaohusu Tunda la mti wa Ujuzi wa mema na mabaya nikawa na mengi ya kuandika na nikasema tuongeze maarifa zaidi kupitia Uzi wangu huu ulio Mrefu.
Niombe radhi kwamba mimi sio mbobezi kwa uandishi ila ukinisoma vizuri utanielewa.


MWANZO 1.16-18 “”AND GOD MADE THE TWO GREAT LIGHTS, THE GREATER LIGHT TO RULE THE DAY, AND THE LESSER LIGHT TO RULE THE NIGHT; HE MADE THE STARS ALSO.17. AND GOD SET THEM IN THE FIRMAMENT OF THE HEAVEN TO GIVE LIGHT UPON THE EARTH.18. TO RULE OVER THE DAY AND OVER THE NIGHT, AND TO SEPARATE THE LIGH FROM DARKNESS.AND GOD SAW IT WAS GOOD.’’’’

Nianze kwa kusema Adam na Eva walikula tunda halisi na hawakufanya mapenzi kama wengi tunavyojaribu kujenga hii picha.Na pia kufanya mapenzi sio sababu iliowafanya wajione wako uchi.

Mti wa Uzima na mti wa Ujuzi wa mema na mabaya, ilikuwa miti halisi na yenye matunda halisi.Miti hii miwili iliokuwa katikati ya bustani iliwakilisha eneo la kiutawala katika Ulimwengu wa Roho ulio halisi pia.Ulimwengu wa Roho ndiko aliko MUNGU na pia kuna Eneo dogo analotawala shetani ambalo lilikuwa ni mali ya mwanadamu.Hivyo basi Eneo alilo Mungu liliwakilishwa na mti wa Uzima ila Eneo la pili analotawala shetani liliwakilishwa na mti wa Ujuzi wa mema na mabaya.YESU alikuja kwa dhumuni maalum la kuirudisha hii nafasi alioipoteza Adam na ndio maana ni rahisi kujua kwamba Adam aliumbwa ili awe nani na sehemu yake ilikuwa ipi,,na nafasi yake ilikuwa ipi.Angalia mstari huu hapa chini “”AKAMWEKA MKONO WAKE WA KUUME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO 21.JUU SANA(nafasi ya kwanza ya utawala anapotawala MUNGU) KULIKO UFALME WOTE(nafasi ya pili alioipata Shetani kwa hila)na MAMLAKA NA NGUVU NA USULTANI NA KILA JINA LITAJWALO.)

EFESO 1:18-23 ‘’’Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru,mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo;na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,19. na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo, kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake 20.aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu,AKAMWEKA MKONO WAKE WA KUUME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, 21 JUU SANA KULIKO UFALME WOTE, NA MAMLAKA NA NGUVU,NA USULTANI,NA KILA JINA LITAJWALO,WALA SI ULIMWENGUNI HUMU TU,BALI KATIKA ULE UJAO PIA.

Unapata picha gani??

Ili kuutawala ulimwengu wote YESU aliketi mkono wa kuume wa Mungu juu sana(ndio sehemu MUNGU alipoketi kinafasi katika ulimwengu wa roho)Sasa hii nafasi ilikuwa ya Adamu tena akiwa pale kwenye bustani ya Eden kabla hajakiuka masharti..Ili Adam aweze kutawala hili eneo dogo lililowakilishwa na mti wa Ujuzi wa mema na mabaya ilimpasa kuwa na ujuzi wa kulitawala kuanzia kwenye ulimwengu wa roho..Utaona ile kula matunda ya mti wa uzima na MUNGU kumtembelea kila wakati wa jioni kuna kanuni,taratibu na mipangilio ambayo MUNGU alikuwa akimfundisha Adamu kwa ajili ya kuweza kutawala.Ninaamini kwamba Mti wa uzima Adam na Eva walikula matunda yake na pia mti wa ujuzi wa mema na mabaya kuna kusudi MUNGU alikuwa nalo katika ule mti na ilimpasa Adamu elimu ili aweze kujua makusudi ya matunda ya mti ule maana haukuwa pale kwa bahati mbaya ila ulihitaji muda, maana Adam alikuwa akiandaliwa kuwa mtawala wa dunia nzima katika bustani..Ukipitia UFUNUO 22:1-2 Utaona kufanana kwa eneo la bustani aliokaa Adam na mahali ambapo hukaa kiti cha enzi cha MUNGU tena kukiwa na mti wa uzima.Hii ni kukuonyesha mti una nafasi katika eneo lililokuwa la kiutawala..Lakini mti wa UJUZI WA MEMA NA MABAYA ulikuwa na muunganiko na eneo dogo la ulimwengu wa roho ambalo lina uhusiano na giza.Ambalo eneo hili lilikuwa salama kabla Shetani hajapata nafasi ya kulitawala..Eneo hili ndilo Lilikuwa nafasi ya Adamu na pia lenye uhusiano mkubwa na dunia yetu,,Ili Adam aweze kuwa Adam ambaye angekuwa mtawala kamili wa dunia alipaswa kulikamata na kulitawala eneo hili kwanza.Na bila shaka mti huu wa Ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa moja ya funguo muhimu za kulifikia eneo hili,,, ila ilimpasa kujua kanuni,taratibu na sheria zilizouhusu mti huu.

Efeso 2:4-6”””Lakini MUNGU, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliotupenda, 5.hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani tumeokolewa kwa neema. 6.Akatufufua pamoja nae,AKATUKETISHA PAMOJA NAE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,KATIKA KRISTO YESU.




1Wakorintho 15:20-26’’’’lakini sasa KRISTO amefufuka katika wafu,limbuko lao waliolala. 21.Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu,,kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.22.Kwa kuwa kama katika Adam wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa(made alive)..24. Hapo ndipo mwisho,atakapompa Mungu Baba ufalme wake;atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote na nguvu. 25. MAANA SHARTI AMILIKI YEYE, HATA AWAWEKE MAADUI WAKE WOTE CHINI YA MIGUU YAKE.26.Adui wa mwisho atakaebatilishwa ni mauti.

Kwa nini mistari hii?

Adam Aliambiwa siku akila matunda ya mti wa ujuzi hakika atakufa,,kifo hichi hakikuwa kifo cha hapo hapo kwamba akila angeanguka na kufa,,ila kilikuwa kifo cha roho yake iliokuwa imeungana na ulimwengu wa roho.Kwamba angeipoteza nafasi yake ya kuketi na MUNGU katika eneo la juu sana ambapo ndio lilikuwa la muhimu kwa Adam kuweza kuwa na uwezo wa kutawala eneo la chini lililowakilishwa na mti wa Ujuzi wa mema na mabaya..Ukimwangalia Yesu utaona kuhuishwa,,sio kwa mtu alie kaburini,,ila mtu anaeishi,,maana yake ni kwamba ile roho ya binadamu iliokosa access ya kuwa kwenye ulimwengu wa roho inarudishiwa ile access kwa kuhuishwa na kuketishwa pamoja KRISTO Katika eneo la juu sana katika ulimwengu wa roho kiutawala..Kwa hio haya yote anayoyafanya YESU ni kurejesha alichopoteza Adamu na pia kukuonyesha ni nini iliokuwa nafasi ya Adamu kiutawala.

Isaya9:1-2’’’Lakini yeye aliekuwa katika dhiki hatakosa changamko.Hapo kwanza aliingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa,lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu,karibu na njia ya bahari;ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa.2.WATU WALE WALIOKWENDA KATIKA GIZA(UFALME) WAMEONA NURU KUU(UFALME);WALE WALIOKAA KATIKA NCHI YA UVULI WA MAUTI NURU IMEWAANGAZA(UFALME wa NURU unachukua nafasi kwenye maeneo ya ufalme wa giza)

Katika bustani ya Edeni kulikuwa na hila na mashindano ya kutawala au kushika nafasi muhimu zenye kuleta uongozi au kuwa na hatua yakuanzia katika kushika maeneo mengine makubwa na muhimu..Unaona giza linawakilisha alama muhimu ya ufalme unaotawala katika ulimwengu wa roho, pia nuru ni alama ya ufalme mwingine wenye kutawala ulimwengu wa roho pia.MUNGU alitaka Adam awe Mungu mdogo wa dunia au mwakilishi wake mwenye nafasi kubwa katika dunia.Ila alikuwa akimtrain ili aweze kuimudu hio nafasi jambo ambalo Ibilisi aliliharibu kwa makusudi mazima kabla halijapiga hatua maana alijua asingekuwa na nafasi yoyote na angekuwa chini ya mwanadamu kimamlaka na kiuwezo.Na ile kuwa na miti miwili ilikuwa ishara ya utawala wa MUNGU na binadamu,,,kwamba Adam alihitaji kuwa na MUNGU karibu ili aweze kutawala,,au utawala/ufalme/nafasi ya Adamu alihitaji utawala wa MUNGU ili aweze kuimarika na kukimudu kiti/nafasi yake.

Isaya14:13-17 ‘’’Nawe ulisema moyoni mwako,Nitapanda mpaka mbinguni,Nitakiinua KITI CHANGU JUU kuliko nyota za MUNGU,nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,katika pande za mwisho za kaskazini.14.Nitapaa kupita vimo vya mawingu,NITAFANANA NA YEYE ALIE JUU.


Napenda ujue hivi Shetani hakuwa na shida ya kufanya mapenzi na Eva,,kitu cha kwanza alitaka nafasi ya mwanadamu katika Ulimwengu mdogo wa roho ili aitimize nia yake aliokuwa nayo kuanzia mwanzo ya kumpindua MUNGU na yeye ashike nafasi ya MUNGU na atawale mbingu na dunia na vilivyomo. Katika bustani ya Eden aliiona fursa ya kulitimiza lengo lililomo kwenye nafsi yake, kuanzia siku alipoasi akiwa kerubi aliekuwa na kazi ya kuufunika uso wa MUNGU Katika bustani ya Adeni ilioko mbinguni.Kila wakati Adamu na Eva walikula matunda ya mti wa uzima na wakawa ni viumbe ambao hawakuwa na hali ya kufa ila walikuwa ni viumbe wa kuishi milele.Na matunda yale yalikuwa ni kiungo cha wao kuweza kuishi sehemu mbili kwa wakati mmoja.Adam alikuwa kama ghost(kwamba mwenye roho yenye uhai iliokuwa na muunganiko halisi na sehemu ya juu sana ya ulimwengu wa roho wenye kiti cha enzi cha MUNGU).Naweza kusema roho ya Adam ilikuwa na nguvu na uhai kiasi kwamba alikuwa ni roho zaidi ya binadamu na ndio maana kule kuwa uchi hakuona ni jambo la ajabu,,same apllied to Eva,,walikuwa ni kama ghost.Kitendo cha Adamu na Eva kula yale matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya kilikata ule muunganiko waliokuwa nao na Eneo la juu sana La MUNGU katika ulimwengu wa roho na wakawa reduced kuwa binadamu wa kawaida asie na uwezo wowote.Na akapoteza nafasi yake.Mungu kumuuliza uko wapi si kwamba hakujua yuko wapi,,, ni kwa sababu hakumwona kwenye nafasi aliokuwa amemuweka.

Waefeso 6:12 “”KWA MAANA KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA; BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Je!! Tuna shindana kwa ajili ya nini?

Kuna kitu tuliibiwa, tulinyang’any’wa tunatakiwa tukipate,,hatujakamilika kwa maana ukamilifu wetu uko katika nafasi alioiiba shetani,,ukimwamini YESU Unaihatarisha nafasi ya shetani katika sehemu yetu alioiiba na unakuwa umemtangazia vita (na atapigana na yeyote Yule ili amaintain hii nafasi maana anaijua umuhimu wake) maana hataki kuiachia kabisa ndio sehemu inayomfanya awe na nguvu,,kwamba ukihitaji mafanikio kimaisha mpaka uhangaike na utoke jasho.Lakini haikutakiwa iwe hivyo, maana shetani aliiba nafasi ya Adam akapata nafasi ya kututawala na akapata njia ya kujaribu kurudi apigane na MUNGU tena kwa wazo kwamba atatimiza nia yake aliokuwa nayo toka zamani ya kumpindua MUNGU na yeye ndo awe MUNGU.Hapa Falme na mamlaka kwenye huo mstari ndio nafasi mwanadamu alitakiwa atawale,,awe na ufalme na mamlaka yake,,,maana huwezi tawala dunia ya kawaida bila kuanzia kwenye ulimwengu wa roho.Na hakuna kitu kilicho kwenye ulimwengu huu wa kawaida kisichokuwa na chanzo kwenye ulimwengu wa roho,,kwa hio ile miti miwili uhalisia wake ulikuwa kwenye ulimwengu wa roho.Shetani anajua sheria anazotembelea MUNGU kwa hio yeye hawezi kumwaribu binadamu ila humdanganya ili binadamu ajiharibie mwenyewe,,hivyo asingefanya mapenzi na Eva kumharibu maana anajua reaction ya MUNGU katika hili.Ila alimdanganya na akaichukua nafasi yao,,maana walishindwa kusimamia sheria walioambiwa na MUNGU. Shetani anajua kwa usahihi maana ya kuvunja sheria ya MUNGU kwamba hutaacha kuwa na gharama ya kulipa.

Namalizia na mstari huu,,mstari wa kwanza wa Genesis nilionukuu na huu wa mwisho wa ufunuo ina kitu cha kufikirisha kuhusu usiku maana ile mianga miwili haikuwa ya kawaida ina namna inawakilisha nafasi..Ufunuo wa Yohana21:23’’’’Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza,kwa maana utukufu wa MUNGU huutia nuru,na taa yake ni mwana kondoo’’’Huu mstari unaonyesha baadae kukiwa na utawala mmoja tu wa MUNGU.

UFUNUO 22:5’’ WALA HAPATAKUWA NA USIKU TENA; WALA HAWANA HAJA YA TAA WALA YA NURU YA JUA; KWA KUWA BWANA MUNGU HUWATIA NURU NAO WATATAWALA HATA MILELE NA MILELE.’’’

LOEB SINCLAIR MPALASINGE.



 
Back
Top Bottom