Johny Mkalawa
New Member
- Jul 14, 2021
- 4
- 1
TURUDISHE TABASAMU KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI.
Picha na: www.shutterstock.com
Kuelekea Tanzania tuitakayo ni muhimu kuandaa Sera, Sheria na Mipango ambayo itawalinda na kuwarudishia Tabasamu watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism).
Hakika ni Aibu kubwa kwa Taifa ambalo lina Miaka zaidi ya 60 tangu kupata uhuru kuendelea kuwa na jamii isiyokuwa na uelewa au yenye uelewa mdogo kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi.
Ni wakati sasa wa kutambua kuwa Ulemavu wa ngozi siyo ugonjwa wa kurithi wala siyo chanzo cha utajiri au bahati bali kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa maarifa na bidii ili aweze kuishi maisha bora.
Watanzania wamepoteza tabasamu na furaha kutokana na Matukio ya Kikatili yaliyotokea hivi karibuni.
(i) Tukio la Mwanafunzi Kazungu Julius wa Shule ya Msingi Katoro-Geita kujeruhiwa maeneo ya kichwani, mkononi na kwenye kidole.
(ii) Tukio la mtoto Noela Asimwe kutoweka Mei 30, 2024 na baadaye mwili wake kupatikana Juni 17, 2024 akiwa ameuawa.
- Haya ni matukio yaliyoacha majonzi makubwa kwa Familia, jamii pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kuelekea Tanzania Tuitakayo ni lazima Serikali, Jamii na Asasi za Kiraia zishirikishwe katika kuandaa Sera, taratibu na sheria za makusudi ili kudhibiti matukio ya namna hii.
Pamoja na hayo katika kurudisha tabasamu kwa Watu wenye Ulemavu wa ngozi mambo haya lazima yafanyike:-
1. Serikali kuwatambua watoto wanaozaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi. Ni muhimu kuwe na kanzidata ambayo itasaidia ufuatiliaji kutoka ngazi za chini za mamlaka kwaajili ya ufuatiliaji na kufamu usalama, mazingira wanayoishi na huduma wanazopata.
2. Kuwawezesha kiuchumi, kimitaji na kielimu ili kuwafanya wawe na maisha salama kiakili, kiuchumi na kijamii.
3. Kutoa elimu ya mara kwa mara kwa Jamii. Elimu kuhusu ukatili na kuwalinda watu wenye ulemavu ipewe mkazo kwenye mitaala ya Elimu kwa ngazi zote. Jamii pia ipatiwe elimu ya kuwalinda watu wenye ulemavu katika kila mkutano wa robo mwaka unaofanyika.
4. Kuwatambua na kuwafuatilia waganga wote wa Tiba Asili. Zoezi hili liwe la mara kwa mara ili kuwabaini Waganga wanaokwenda kinyume na leseni zao. Na wakibainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
5. Hukumu kwa waliofanya ukatili kutolewa Mapema. Baada ya zoezi la upelelezi kumalizika watuhumiwa wote wapelekwe mahakamani na kuhukumiwa haraka kuliko kuchelewesha hukumu na kuibua maswali miongoni mwa watanzania.
Yote hayo yakifanyika kwa usahihi na usimamizi ni imani yangu kila Mtanzania hasa wenye ulemavu wa ngozi watarudisha tabasamu na kujiamini ikienda sambamba na kuishi katika Tanzania salama na Tanzania Tuitakayo.

Upvote
4