Mkumba Ndanda
New Member
- Aug 9, 2022
- 2
- 1
Nchi nyingi za Afrika mara baada ya kuhodhi uhuru wao kutoka kwa wakoloni zilikichagua kilimo kama sekta kuu ya maendeleo ya kiuchumi, na kukisanifisha kama UTI WA MGONGO WA UCHUMI wa nchi zao.
Nchi huru za Afrika zilikuwa na sababu sufufu za kukifanya kilimo kuwa nyenzo kuu ya uchumi, licha ya kutoshabihiana katika hali za kimazingira, kitamaduni na hata kiuchumi lakini nchi zote zilijikuta ndani ya kizingiti chenye sababu tatu shiriki zilizorasimisha kilimo kuwa sekta kuu ya maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao.
Mosi, kilimo ni tunu pekee ya mfumo wa uzalishaji ambayo ilirithiwa na mababu zetu tangu kale, ni kilimo pekee ambacho kiliweza kuwapa fursa waafrika kushiriki katika nyanja hai ya uzalishaji katika enzi za Ukoloni, wakoloni walitambulisha mazao mbali mbali kwenye nchi mbali mbali barani Afrika huku wakitumia kilimo kama chanzo cha uzalishaji wa chakula na malighafi mbali mbali kwa ajili ya viwanda vyao pamoja na hilo kilimo kilitumika kama nyenzo ya kuinyonya nguvu kazi ya Afrika.
Pili, sekta ya kilimo ilichukuliwa kama sekta nyepesi kuanza nayo kuelekea maendeleo ya kiujumla ya kitaifa, hii ilichagizwa na mahitaji madogo ya mtaji kwa ajili ya shughuli za kilimo kulinganisha na sekta ya viwanda na uwekezaji kwa ujumla wake, pia msisimko ulioibuka juu ya kilimo cha jadi ambacho kilifanywa na kaya mbali mbali kwenye maeneo yao waliyoyamiliki ulichochea kwa kiasi kikubwa kukirudufisha kilimo kwenye nchi nyingi za Afrika huku familia hizo zilikua zikitumia zana duni katika shughuli hiyo kutokana na usawa wao mfu wa kifedha.
Tatu, wazee wetu waliamini kwamba sekta hii mama haikuhitaji utaalamu mkubwa kwenye hatua za awali tofauti na sekta nyinginezo lakini pia kwa mujibu wa hekaya za kale wakoloni walikua wakiwapa taaluma mbali mbali za uzalishaji waafrika ambao kwayo waligeuka kuwa vibaraka wa wakoloni hivyo hawakuwa na mchango wowote kwenye jamii yao pia taaluma kuu zilizokua zinatumika katika nyanja kuu za uzalishaji kamwe hazikuwahi kutolewa kwa waafrika, hivyo hakukua na namna nyingine yoyote zaidi ya kilimo.
Tanzania kama ilivyokua kwa baadhi ya nchi nyingi barani Afrika mara baada ya kupata uhuru wake kutoka kwa Waingereza mnamo Disemba 9, 1961 wakati huo ikiitwa Tanganyika na baadae kulitwaa jina la Tanzania baada ya Muungano wa serikali ya Tanganyika na ile ya mapinduzi ya Zanzibar, iliazimia kama nchi kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa.
Kilimo kikachukua sura yake kwenye ardhi ya Nyerere, kila kona ya nchi jembe lilihubiriwa sana, si wanaume wala wanawake yeyote mwenye nguvu thabiti alijikatia shamba na kulihudumu kadri awezavyo taaluma duni ya ukulima ikatawala kwenye ukanda mkubwa nchini na kwa kiasi kikubwa kilimo cha chakula kiliimeza sekta ya kilimo cha biashara ambayo haikua na nguvu labda kutokana na mwamko wa watu au kiasi cha mtaji kilichohitajika kwa ajili ya kilimo hicho.
Hata lilipopita azimio la arusha mwaka 1967 ni kilimo ndicho kilichotambulika kama nyenzo ya kujikwamua kutoka katika umasikini na kuleta chachu ya maendeleo nchini, maeneo maalumu yaliyotambulika kama vijiji vya ujamaa yalitengwa kwa ajili ya shughuli mbali mbali za uzalishaji huku kilimo kikisimama kama shughuli kuu ya uzalishaji sambamba na ilo nguvu kazi ilikusanywa kutoka mijini na kwenda huko vijijini mahsusi kwa ajili ya kufanya shuguhuli hiyo ya kilimo hapa ndipo kundi kubwa la vijana waliokua hawana kazi maalumu mjini waliolowea kucheza drafti na bao la kete walikusanywa kupitia magari ya serikali na kupelekwa kwenye vijiji vya ujamaa.
Hadi leo hii bado kilimo kimekuwa muhimili mkubwa wa uchumi wa taifa letu kikihuishwa kila baada ya miaka kadhaa kwa sera mbali mbali kama vile “kilimo kwanza”.
Licha ya harakati zote hizo bado hainiwii vigumu kusema ya kuwa hatukujipanga wala hatukuamua kuirutubisha sekta ya kilimo kufikia maudhui yale tuliyoyanasibisha na sekta hii ya kuifanya kuwa nyenzo kuu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini, hii ni kutokana na msururu wa changamoto lukuki zinazoiandama sekta ya kilimo nchini.
Kwanza hatukuweza kuamua juu ya zao kuu, zao la taifa ambalo lingeitambulisha nchi kwa nafasi yake huku likivutia uwekezaji kutoka sehemu mbali mbali, mfano katika nchi ya Ghana wao walijipambanua vilivyo kupitia zao la Kakao ambalo kwa kiasi kikubwa liliipa nguvu sekta ya kilimo nchini humo nakuchagiza maendeleo kwa jamii husika kutokana na idadi kubwa ya ajira zilizopatikana kutokana na kilimo hicho cha taifa hilo.
Lakini pia nchi yetu haikuweka misingi stahiki ya kukuza kilimo kuanzia katika ngazi ya chini kabisa ya wakulima wadogo wadogo, hakukuwa na mfumo thabiti ambao ungewawezesha wakulima kuachana na zana duni na kuhamia katika zana bora na za kisasa za kilimo, ni ukweli usiopingika kuwa vifaa vya kilimo cha kisasa ni ghali lakini serikali ilikua na uwezo wa kuingia na mikataba na makampuni mengi ya uzalishaji wa vifaa vya kilimo kisha mikopo nafuu ya vifaa vya kilimo yenye kuangalia kipato cha mkulima mdogo ingetolewa huku kukiwa na makubaliano baina serikali na wakulima juu ya marejesho ya mkopo huo bila kuathiri maslahi ya mkulima na uchumi wa nchi.
Pia nchi yetu haikuweza kustawisha benki nyingi za kilimo, sawa kwasasa ipo benki ya maendeleo ya kilimo nchini lakini kutokana ya kuwa kilimo ndio shughuli inayofanywa na watanzania wengi nadhani serikali ilipasawa kustawisha benki za kilimo nyingi zaidi au la benki hii ingejigawanya na kufanya kazi zake kikanda kwa mfano kungekua na tawi la kanda ya kusini, kanda ya kati, kanda ya ziwa na kanda ya pwani ya mashariki hio ingesaidia sana kuwafikia wakulima kwa ukaribu zaidi na kuwapatia huduma ya mikopo yenye gharama nafuu kwa ajili ya mtaji ili kuongeza uzalishaji kwa ufanisi mkubwa.
Na pia sio mbaya kama kungekua na benki zilizohai kwa ajili ya vilimo teule kama vile benki ya kilimo cha korosho, benki ya kilimo cha chai, benki ya kilimo cha pamba, benki ya kilimo cha mpunga na hata benki ya kilimo cha mahindi, benki hizo zingesaidia kukuza vilimo husika katika nyanja ya uzalishaji na ubora wa mazao.
Tamati ya yote elimu pana inapaswa kutolewa juu ya uzalishaji wa bidhaa tofauti tofauti kutokana mazao mbali mbali ili kukuza ukubwa wa soko la bidhaa zitokanazo na kilimo ili tuweze kukifanya kilimo kuwa uti wa mgongo wenye rutuba na tija kwenye maendeleo ya uchumi wa taifa letu.
Ndimi Mkumba Ndanda Mjugumbi[emoji871]

Upvote
1