Tusahau katiba mpya

Tusahau katiba mpya

Mjomba Mkude

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2013
Posts
287
Reaction score
110
Wadau nimejaribu kufikiri uwezekano wa Watanzania kupata Katiba mpya kupitia mchakato huu unaoendelea na kwa tathmin yangu naona hatutopata katiba mpya..nina sababu..
1.CCM na washirika wao lazima watapitisha serikali mbili bungeni hii ni kutokana na wingi wao.
2. Wakati wa kupiga kura wananchi watakataa mfumo huo wa serikali mbili na kutokana na sheria ya mabadiliko ya katiba kwamba wananchi wakipiga kura ya hapana basi katiba ya 77itaendelea kutumika.
MaCCM yataibuka mashindi.
.Vinginevyo Either katiba mpya yenye serikali 2 au Katiba ya mwaka 77.
Tungoje tuone.
 
duu hapo kaz ipo kwa.kweli..ila mm kinachoniuma ni kwamba, hilo daftari la kudumu linaboreshwa lini jamani? wengine kama mimi tuliopoteza kitambulisho cha.mpiga kura tunakosa haki yetu ya msingi hata hivyo vitambulisho vya uraia vitatufikia kweli? ili tuweze kuvitumia katika kura ya maoni?
mbona wanalegalega na hili zoezi jamani?
 
Hapa nimejua tu ,na haswa baaada ya kuisikiliza hotuba ya Mh.Kikwete ,kama utaisikiliza kwa makini sana ,utagundua kitu ambacho Mheshimiwa alikuwa akikirudiarudia ,..hakutopatikana kitu....kwa ufupi akituhabarisha kiujanja ujanja kuwa hakuna cha katiba wala kanuni ,yaani hakuna makubaliano yatakayopatikana ,huu ni msimamo wa CCM akiuwakilisha kiaina ,unaweza usione chochote kwa jinsi alivyoisuka ,ila kwa upande wangu mimi binafsi nilihisi tayari nimeshapata jawabu la kuwa hakuna kitakachopatikana ni babaisha na gelesha tu itakayofanyika.
 
Back
Top Bottom