Hapa nimejua tu ,na haswa baaada ya kuisikiliza hotuba ya Mh.Kikwete ,kama utaisikiliza kwa makini sana ,utagundua kitu ambacho Mheshimiwa alikuwa akikirudiarudia ,..hakutopatikana kitu....kwa ufupi akituhabarisha kiujanja ujanja kuwa hakuna cha katiba wala kanuni ,yaani hakuna makubaliano yatakayopatikana ,huu ni msimamo wa CCM akiuwakilisha kiaina ,unaweza usione chochote kwa jinsi alivyoisuka ,ila kwa upande wangu mimi binafsi nilihisi tayari nimeshapata jawabu la kuwa hakuna kitakachopatikana ni babaisha na gelesha tu itakayofanyika.