Tusaidiane kubuni Jina la biashara

georgeallen

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
4,118
Reaction score
1,875
Wandugu, ili kujikomboa na halii hii ngumu ya maisha iliyotunyemelea hapa nchini miaka hii, mwenzenu nimejipigapiga na kufanikiwa kujenga mjengo kwa ajili ya biashara ya nyumba ya kulala wageni, bar, na mgahawa. Majengo ya biashara hii yapo kando kando ya moja ya barabara kuu za Tanzania na muda si mrefu itaanza kazi. Tatizo langu kubwa kwa sasa ni jina gani litabamba kwa hii biashara na ukweli ni kuwa kila jina ninalolifikiria naliona kama siyo au tayari linatumika sehemu fulani huko duniani. Majina kama Dynasty club, Ecape six, Elewana, oriental resort, Highway comfort, Hillside hideaway, Palmview motel, Hillsview inn, Darway motel, africana, Bell air, Mel rose Place au hata "Mara lago club" la yule babu anayewania urais USA yote yameishachukuliwa au siyo mageni tena kwenye masikio ya watu. Ni kwa sababu hizo na nyingine za kibiashara au kisheria basi nakuja kwenu kuomba msaada wenu kubuni jina la biashara yangu hii.
 
Ipe hili hapa KANIITIE COMPLEX BAR (KCB).
 
Chagua hapa
KENZY HOTEL
Lzm nijipendeleeπŸ˜€
DIAMOND HOTEL
watu watajua ni ya diamond hivyo wataishobokea!
MOON LIGHT HOTEL
DAR CITY HOTEL
ukikosa hapo iite kauli mbiu ya mkulu..πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kha, hili jina litakuwa balaa na hasa hawa -TGNP na TAMWA- wataondoka na kichwa changu.
Kwanini mkuu..! Nimejituma kukupatia hili jina kutokana na fani yangu. Lifikirie mara mbili mkuu.
 
nimeongeza: Ugalimoto "nyama choma" Pub au Hot meal BBQ pub
Mkuu watu wengi huwa hawajui tofauti ya Hotel, Restaurant, Food Court, Motel n.k. anyways kwa muda wako utapitia kuona tofauti zake!
Lakini pia kuna haja ya kujielimisha kidogo juu ya jina zuri la biashara liwe na sifa zipi, unique, simple, lisilo sahaulika, liwe na image yako, familia, taifa n.k
... fikiria aliyebuni jina la migahawa ya "McDonalds"simple as that lakini habari yake sote tunaijua...
 
Chagua hapa
KENZY HOTEL
Lzm nijipendeleeπŸ˜€
DIAMOND HOTEL
watu watajua ni ya diamond hivyo wataishobokea!
MOON LIGHT HOTEL
DAR CITY HOTEL
ukikosa hapo iite kauli mbiu ya mkulu..πŸ™πŸ™πŸ™
Hili la kauli mbiu ya ngosha aka mwendokasi nimelichukua na nimelipa grade za juu. Thanks
 
yangu ni motel ila kwenye compound hiyo kuna bar na restaurant, nataka jina liwe unique, simple, captivating kwa mfano: escape one, landmark, pure heaven, four seasons, oriental etc
 
We unaweza kujiaribia kwa upande wa pili(upinzani)πŸ˜€
Kenzy? hapana-utaniburuza kwa pilato( litigation) na msingi wenyewe huu nimekopa kwa kimei ndiyo nitaingia moja kwa moja kwenye ile ratio ya 1:4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…