Tusaidiane kuhusu kilimo cha bustani ya mipapai

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Habarini wadau! kheri ya mwaka mpya!!

Kuna ndugu yangu kamaliza chuo mwaka juzi. Mama mnavyojua, suala la ajira ni kitendawili kilichokosa majibu. nimefikiria kumshauri aanzishe tu kijikibustani cha mipapai ili aweze kujipatia chochote baada ya muda.

Kaeneo kalichopo ni kama robo tatu ekari tu. Sifahamu sana kuhusu kilimo hicho lakini akili yangu inahisi kuwa ni chenye tija tu. Dogo, kwakuwa amevurugwa, hana neno kwenye hilo, anahitaji mtaji tu.

Sasa wadau, kwa mwenye ujuzi, naomba anipatie somo kidogo kuhusu uanzishwaji wa bustani kama hiyo, faida, hasara, masuala ya mtaji na kuhusu eneo langu pendekezwa kama lina tija.

ahsanteni na mbarikiwe sana!
 
Ngoja nikuitie mdau katika zao hilo mkuu Matola pengine atakupa mawili matatu of vital importance...!
 
Mimi nakupa uzoefu wangu wa field,

Robo tatu ya ekari ni eneo kubwa sana kwa kilimo cha papai, kama atakuwa serious na akapoteza muda wake mwingi na nguvu zake huwenda asitamani tena ajira ya mtu.

Habari wakulima na wafugaji wenzangu, kumekuwa na malalamiko mwengi siku hizi kwa wakulima wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo cha papai kwamba wanakutana na mipapai dume mingi pindi wanaponunua miche ya mipapai kutoka kwa wazalishaji wa vitalu ya miche hiyo.

Siku hizi watu wamekuwa sio waaminifu, mtu anaweza kununua papai sokoni bila kujua aina ya mbegu akaja akaotesha miche kisha akaipachika jina lolote analojua yeye halafu akauzia watu, papai likishachakachuliwa mara nyingi lazima lipungue ubora na pia lazima upate mipapai dume mingi hata 50 kwa 50 kwani mbegu hybrid lazima ipatikane mbegu yenye sifa ya kike na ya kiume kwa hiyo kama itachakachuliwa sana inarudi kwenye sifa zake za awali.

NINI CHA KUFANYA?
Kama unataka kuwekeza kwenye kilimo cha papai na uwezo wako ni mdogo, nenda kwenye duka la pembejeo linaloeleweka nunua mbegu chotara inayojulikana hata ya Tsh 15,000 kisha otesha miche yako mwenyewe uitunze kwa uangalifu, ikishaanza kuzaa hapo unaweza kuchagua mipapai bora ukaotesha kitalu chako unachohitaji na idadi ya miche yoyote unayotaka. Hapo miche yako itakuwa ni bora kwani huo ni uzazi wa kwanza hivyo inakuwa haijapoteza ubora wake kwa kiasi kikubwa.

JINSI YA KUPANDA MICHE YA PAPAI SHAMBANI

Chimba shimo la Futi mbili upana na Futi mbili urefu

Weka mbolea yako ya samadi angalau ndoo ndogo mbili kila shimo

panda mche wako wa papai

Kama eneo lako halina maji ya kutosha panda miche yako wakati wa masika

MAKADILIO YA MAPATO

Robo Tatu ya ekari inaingia miche 750 kama shamba limepandwa Kitaalamu ila kwa mashamba yetu ya uswahilini kadilia miche 500

Chukulia mche mmoja umezaa papai 20 ingawa Kitaalamu ni miche 40

20 *500 =10000

Chukulia umeuza papai moja Tsh 300 hapo hapo shambani

10000 *300 =3000000

Kumbuka huo ni kwa uzao mmoja na tumeweka papai 20

Kumbuka kwa Mwaka inaweza kuzaa hata mara 3

Huu utaalam ni wa field mimi mwenyewe ndio nimeanza kilimo hiki

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hii baishara sasahivi inaendeleaje..naona kama watu wamekata tamaa kuwekeza
 
Asante kwa elimu
 
Umbali gani unaweza kupanda kutoka mpapai mmoja mpaka mwingine na jee sehemu za bondeni zenye udongo mfinyazi ambazo hupita maji kipindi cha mvua inawezekana kustawisha vizuri zao hili?
 
Back
Top Bottom