Gill Rugo
Member
- Aug 28, 2022
- 30
- 121
Naikumbuka bayana siku hiyo. Hususani ule mlio, mkubwa kuliko kumbukumbu yenyewe. Nilikua mdogo sana lakini nakumbuka dhahiri kila kitu. Ni moja kati yale matukio unayobeba akilini mpaka kifo. Yale matukio tambuzi yanayoathiri mustakabali wa maisha yako. Na ndio maana sielewi! Sielewi kwanini mama anashangilia. Anaonekana mwenye furaha. Watu wote hapa wana furaha! Naakisi ‘WAMEMPATIA NAFASI NYINGINE’.
Nilikua mwenye miaka saba tu. Alikua gavana wetu huyu. Mzozo ulihusu Bilioni saba zilizopotea bila mahesabu. Yaani saba yenye zero tisa mbele yake! Nakumbuka niliperuzi tena inshu hiyo mtandaoni kabla sijakutana na ponografia. Alibanwa sana huyu. Kiasi cha kukosa majibu.
Ghafla! Pa!
Alimpiga shaba mtu. Tuliona wote, mubashara kwenye runinga. Gavana wetu akimpiga risasi mwananchi. Ilikua kama sinema ya mapigano nisiyoielewa, sinema ambayo unaweza kusema jambazi ni huyu aliyesimama jukwaani leo. Mama alipozima runinga, ukimywa ulitawala. “SIASA WAACHIE WANASIASA” baba husemaga. Amerudi tena leo, yuleyule gavana wetu, anataka kura zetu kwenye kinyanganyiro cha uraisi. Baba anasema tumpe kura kwa sababu ni 'mwenye nguvu', 'anaogopwa', pia ni “MTU WA KWETU”. Kura yangu nitampa . Najua mnahisi ni kwa sababu baba amesema lakini ni kwa sababu…....... sawa nitakua mkweli, ni kwa sababu ‘BABA AMESEMA’.
Mjomba yeye haamini katika nguvu. Anaiabudu sana akili. Anadai siasa za mabavu zimeshindwa kutatua matatizo yetu. Hivyo tubadili sera zetu. Tutafute mitazamo mbadala kwa ajili ya matatizo haya. Kwa mfano kuna siku dada alikuja kavaa kimini. Mama alikasirika sana “NI KINYUME NA MAADILI YETU YA KIAFRIKA” alidai, na pia 'inawatega wanaume'. Mjomba hakupenda hilo, anadai dawa ni kuwafundisha wanaume kuheshimu miili ya wanawake, sio kuthibiti mavazi ya wanawake. Nilicheka sana hiyo siku. Kwa kiasi nahisi mjomba yuko sahihi.
Baba anasema tusimsikilize mjomba, “WAKOLONI WAMEMSHIKA AKILI”. Mimi nadhani ni uwoga tu, uwoga wa mabadiliko kwenye familia yangu ya kihafidhina. Angalia jinsi tunavyopenda kusema ‘mila zetu za kiafrica’. Ndio sisi ni wamoja katika uonevu tuliopitia kutokana na ukoloni lakini sisi ni jamii tofauti zilizokua katika Nyanja mbalimbali. Kusema 'mila za kiafrika' ni kujumuisha tamaduni na mila kedekede za mataifa mbalimbali kuwa kitu kimoja, kutupa utambulisho ambao wabaguzi waliutumia ili kulitawala bara zima. Mjomba anaamini kwa sasa mila zetu ni mseto wa mila tulizokua nazo kabla ya ukoloni na zile tulizochukua kutoka magharibi. Tulikubali hilo kwanza anamaliziaga. Kwa kiasi pia nahisi yuko sahihi.
Fikiria staili yetu ya mavazi, sanaa yetu na hata vyakula. Vyote ni mchanganyiko wa ukale na umagharibi. Hakuna ambacho twaweza kusema kipo kama kilivyokuwa kabla ya wakoloni. Historia yetu pia ni kwa msaada wa mataifa ya magharibi. Kushikilia utambulisho ambao hatuna ni kutokuitendea haki leo yetu. Ni kuchelewesha adhima yetu.
Ili kukua inabidi kwanza tukubali wapi tulipo. Kuukubali uhalisia wetu bila kujidanganya kwa visasili. Kuzijua nguvu zetu. Kuyaweka bayana mapungufu yetu. Kusema ukweli bila kujari nani utamkera. Ni maneno ya mjomba hayo, mimi sio mwelevu kiasi hicho.
Nadhani ingekua juu yangu nisingempa kura huyu. Nami natamani mambo yabadilike, yacheze hasa kwenye nyanja ya ubongo. Sisi ni binadamu. Tofauti na wanyama wengine sisi tuna welevu, tunaakili ya kuakisi juu ya maisha yetu. Tuna uwezo wa kujua hili ni zuri, lile ni baya. Kulibadilisha jambo fulani baya kama itahitajika hata kama tunaliamini kiasi cha kulifia. Ndio, ukoloni ni unyama mbaya kuliko wote kututokea lakini kuchukua mambo fulani chanya kutoka mataifa ya magharibi au mashariki sio udhalili. Ni maendeleo. Maendeleo yaliyoandikwa kwenye vinasaba vya binadamu.
Lilikua ni swala la mda tu jamii yetu kua ya kidemokrasia, jamii yetu kuuangusha mfumo dume, mavazi yetu kubadilika bila hata ya muingiliano na mataifa ya magharibi. Mkondo wa mda huleta mabadiliko chanya kwenye jamii yoyote yenye ustaarabu. Au labda pia kulikua na jamii zilizoendelea kwenye nyanja mbalimbali za kijamii lakini tunajumuishwa ili kutubagua kwa pamoja, ili kususha maendeleo ya baadhi yetu.
Nachotaka kusema ni binadamu tumeumbiwa mabadiliko. Na sisi hatuwezi liepuka hilo. Mila zetu, haijarishi tunazitukuza kiasi gani zina mapungufu. Mapungufu ambayo kama viumbe wenye akili tunatakiwa kuyasahihisha hata kama itatubidi kukopa elimu kutoka kwa wakoloni wetu. Au kuna mabadiliko makubwa kuliko usawa kwa wote? Kwani kuna madiliko chanya zaidi ya uhuru kwa wote? Najiuliza kama kuna mabadiliko mazuri kuliko yale yanayoondoa umasikini kati yetu. Nadhani hakuna. Unaweza kusema na mimi pia 'wakoloni wamenishika akili' sasa.
Nakumbuka siku mjomba wangu alipoondoka nyumbani. Baba alikua kampiga mama. Bado anampiga. Na bado mama anabaki. Watu kijijini kwetu wanaamini wanawake aina ya mama yangu ni hodari sana. Alienda jando alipokua binti, nasikia wanaambiwaga “ MWANAUME ATAKUPIGA TU KAMA ANAKUPENDA! MWANAUME ATACHEPUKA TU HATA UFANYEJE!”. Dada yangu huamini hivyo pia, Unaweza kusema yeye ni ‘zao la jamii yetu’.
Mjomba aliporudi na polisi nilisema hakuna kipigo chochote kilichotembezwa. Ningesema ukweli lakini mama alinambia kamwe 'nisitangaze mambo ya nyumbani yeyote asiyehusika'. Yuko sahihi sana lakini hata akishikiwa kisu nayo iwe siri? Kwani siruhusiwi kuokoa maisha ya mama yangu? Nadhani sikulelewa kuwa jasiri.
Mjomba yuko sahihi. Inabidi tusasishe mila na tamaduni zetu. Muda umewadia kwa mila kuendana na uhalisia wa nyakati tulizomo. Sio kwamba tuziache kabisa lakini tuweke ukweli, usawa, uhuru, heshima na mantiki ndani yake. Na sio kwamba desturi zetu hazina mambo hayo bali ni kwamba zinahitaji usawa zaidi, uhuru zaidi, heshima zaidi, na mantiki zaidi ndani yake. Yaliyomo hayatoshi kwa kiasi fulani au pia yameelemea upande mmoja. Tukubali kwamba mila zetu ziliandikwa kwa ajili ya nyakati tofauti sana na hizi tulizomo. Dunia imejifunza ukweli mpya, ukweli ambao unatosha kubadili desturi. Nikipata watoto ntawapatia mafunzo aliyonipa mjomba wakiwa angali waduchu.
Ni kutokuyaongelea yanayotokea , kutoyajadili kwa upana, ndiko kunatunyima ukweli juu ya nafasi yetu katika dunia hii endelevu. Imani ya kua wazee hawakosei ndiyo inatuzuia kubadilisha mambo yaliyopitwa na wakati, ndiyo inamuweka mama katika minyororo ya ukatili wa kijinsia. Ni imani ya kua kila mtu anahitaji nafasi ya pili bila kufanya majukumu yake ndio imemrudisha huyu kutuomba kura za uraisi.

Upvote
2