Tuseme kweli: Nani anapenda kumpeleka mwanae Sekondari ya Kata?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mimi nimesoma shule za kata.Hata chuo (IFM) ni kama cha kata!Lakini shuruba katika ufaulu wangu nazijua mwenyewe.

Hapa nataka kusema tuliosoma kule sio kwamba hatuko vizuri kichwani, NO tuko vizuri,ila inalazimu ufanye jitihada kubwa kwenda sawa na wa ki-Mery mery!

Huko kila kitu duni, ila ni kwa sababu umaskini,hakuna namna. Nina uhakika hakuna mtu anayependa mwanae au nduguye asome shule hizi!

Kila mwenye kanafasi anafanya awezalo kumtupa mwanae hata angalau kashule ka milioni apate uelewa! Nadhani lengo lilikuwa zuri,ila kwa kuwa CCM ina hulka ya kushindwa, ikaona isiwe tabu.
 
Me nafundisha ward school.Aina ya wanafunzi tunaopokea ni wale wanaotoka familia dhaifu kiuchumi hata kiuelewa kuhusu umuhim wa elimu,
 
Nimesoma Jangwani Girls na mabinti wawili was Dk Shein kipindi kile ni makamu wa Rais...inategemea
 
Hayo ya kweli mimi pia nimesoma shule hizo hizo, kilichoniuma zaidi nilipofika advance level kwenye somo la geography mery mery wenzetu walikua wameshasoma topic nyingi o level ambazo zipo advance pia.

Kama hiyo haitoshi mwalimu wetu wa physical geography akahama baada ya miezi mitatu tu tangu niingie shule. nilikomaje kwa Mtegetwa., hatukuwahi kufanya mitihani ya kishule tangu siku hiyo hadi mtihani wa taifa.

Baba Mtegetwa MUNGU akuzidishie
 
Nimesoma Jangwani Girls na mabinti wawili was Dk Shein kipindi kile ni makamu wa Rais...inategemea

Siamin kama jangwani ni shule ya kata? Shule za kata nyingi ni zile zilizojengwa kipindi cha Uongozi wa JK kuhudumia wanafunzi wa kata ilipo hiyo shule. ni shule changa sana zenye changamoto lukuki kama upungfu wa walimu, maabara nk
 
Kimsingi kuwa shule ya kata sio hoja. hoja ni je zina mazingira yanayokidhi viwango vya utoaji elimu bora?
Hata shule nyingi tu za private, seminary nk zimechoka sana kitaaluma kuliko hiz za kata.
 
duu kwel kazi huk kigoma ndio mpaka leo dent yuko fm4 ukmulza kuhsu capital leters hafahamu
njoo kwnye lugha sasa wanafunz wote wanaongea kiha kila sehemu shulen ndio ucpme.
sasa mwanafnz kama huyo atatokaje necta

ila dogo anaypga vizur na kutoboa kwnda advance huku shule zet za kata unakta kwel ni kichwa ananyoka direct to unversity level wth upper class

God bless them all.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…