Tushauriane zawadi ya Valentine's Day isiyozidi Tsh 20,000/=

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Kuelekea sikukuu ya wapendao 14/02/2020.

Hebu weka wazo la zawadi unayofikiri utanunua au kuandaa kwa ajili ya mpenzi/mpendwa wako ila bajeti isizidi Shilingi 20,000/=

Kwa kuweka limit ya kiwango hiki pengine itashawishi wengine wanaofikiri zawadi ni lazima iwe ya gharama kubwa.

Inaweza kuwa zawadi ya elfu 1,2,5,10 nk ilimradi isizidi kiwango tajwa hapo juu,lengo ni kuonyesha upendo na kujali bila kuangalia thamani ya zawadi.

N:B Mimi nafikiria kuandaa kuku wa kukaanga kwa kachumbari na Pepsi 1
(Nitaandaa mwenyewe Nyumbani)

Bajeti:

Kuku 1 wa kienyeji. 10,000
Pepsi take away. 1,000
Jumla. 12,000

Karibuni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…