EGF
JF-Expert Member
- Feb 12, 2017
- 387
- 986
Usawa wa kijinsia ni lengo la jitihada za kuleta usawa kati ya jinsia zote, kutokana na dhuluma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine. Usawa wa kijinsia unahusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi.
Waathirika wakubwa katika suala la usawa wa kijinsia duniani kote linawakumba zaidi jinsia ya kike kwasababu tu wanahesabika kama ni viumbe dhaifu.
Hii ni dhana ambayo imejengeka hasa katika jamii za kiafrika. Jamii nyingi zinaamini mwanamke ni mtu anaepaswa kufanya shughuri za ndani pekee na si shughuli za uzalishaji.
Hata hivyo kumekua na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali, mashirika ama vikundi vya watu katika kubadilisha mtazamo hasi kuhusu usawa wa kijinsia na umuhimu wake katika jamii.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekua ikionesha jitihada za wazi za kupambana na uminywaji wa haki za usawa wa kijinsia na kuhakikisha jinsia zote zinaheshimiwa na watu wote bila ubaguzi.
Moja ya jitihada za serikali ni pamoja na kuanzisha sera mbalimbali ambazo zinatoa miongozo ya serikali katika kuwapa wananchi muelekeo wa wanawake na jinsia utakao hakikisha sera, mipango na mikakati na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazingatia usawa wa jinsia.
Hii inatokana na ukweli kwamba majukumu ya mwanamke katika jamii ni tofauti na yale ya mwanaume lakini yote ni muhimu kwa maendeleo ya familia, jamii na Taifa.
Yapo mafanikio mengi yaliopatikana katika utekelezaji wa sera hii ingawa ushiriki wa wanaume umekua hafifu.
Mafanikio hayo ni kama vile kuwepo kwa ufahamu zaidi kuhusu haki za wanawake katika ngazi mbalimbali za kufanya maamuzi na mipango. Uanzishwaji wa mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayolenga kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika Nyanja mbalimbali.
Pia kuwezesha kutambulika kwa michango ya wanawake katika maendeleo yote ya nchi na kupewa fursa zaidi katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za siasa, uongozi, utawala na kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
Katika kipindi cha hivi karibuni Tanzania imeshuhudia ongezeko la idadi ya wanawake katika masuala ya uongozi na kuakisi dhana ya 50/50.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Tanzania iliweza kupata wanawake wabunge 23 waliopata nafasi zao kupitia majimbo ya uchaguzi. Ukijumuisha na wale wa viti maalumu, Bunge la Tanzania likafikisha asilimia 29 ya wabunge wanawake -kiwango cha juu kabisa kwa wakati huo.
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 idadi ya wabunge wanawake ilikuwa imefikia kiwango cha asilimia 37; kikubwa katika historia ya Tanzania tangu Uhuru. Ni wazi kwamba kila wakati takwimu zinazidi kuwa za kuvutia kwa wanawake.
Tanzania sasa inaongozwa na Rais mwanamke mama Samia Suluhu Hassan. Hii inaonesha kwamba wanawake wanao uwezo wa kuongoza nyadhifa mbalimbali katika uongozi na katika hali ya kujiamini kabisa.
Hata hivyo wanawake wameendelea kujitokeza katika Nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya michezo. Mfano mzuri kwa sasa nchi yetu imeanzisha Ligi ya wanawake kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa.
Lakini pia ipo michezo mingine kama vile netball, tennis, riadha pamoja na mchezo wa masumbwi. Hii inaonesha ni kwa namna gani suala la usawa wa kijinsia limepewa kipaombele katika serikali yetu.
Zipo faida nyingi za usawa wa kijinsia ambazo haziishii tu kwa mwanamke bali kila mtu ambaye maisha yake yatabadilika kutokana na usawa kwa jinsia zote mbili.
Mwisho nimalizie kwa kusema
"UKIMUELIMISHA MWANAMKE, UMEIELIMISHA JAMII"

Upvote
0