SoC01 Tushirikiane katika kutokomeza vikwazo vya kimaendeleo katika jamii zetu

SoC01 Tushirikiane katika kutokomeza vikwazo vya kimaendeleo katika jamii zetu

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Ili Maendeleo yawepo panahitajika amani, umoja na mshikamano katika kufanya shughuli hizo zenye kuleta maendeleo katika jamii.

Serikali imekuwa ikiweka jitihada nyingi katika kuhakikisha inathibiti vitendo mbalimbali vinavyoathiri maendeleo ya wanajamii katika kuhakikisha hilo badi inaendelea kuweka sheria mpya mbalimbali ikiwa ni moja kati ya hatua za kudhibiti vikwazo hivyo

Miongoni mwa vikwazo ambavyo jamii na serikali kwa ujumla inavipinga ni pamoja na

1. Matumizi ya madawa ya kulevya ambapo serikali imeendelea kuweka sheria kadhaa kwa wanaokiuka mwenendo wa kiserikali katika kulidhibiti hili

2. Pia ukatili wa kijinsia ni moja ya vikwazo hivyo ambapo kila mmoja anatambua kufanya hivyo ni kosa la jinai hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake kwa maana tunapoona linatokea hili tusilifumbie macho kwa kuwa sisi ni taifa kwa maana ni wamoja katika kutimiza haki na kutetea wanyonge hivyo hili ni jambo la kulipiga vita kwa jamii ili kuiendeleza amani yetu tuliyojiwekea

3. Rushwa, imekuwa ni moja ya vikwazo vya kimaendeleo vinavyochochea umasikini na uonevu katika jamii. Hivyo tunayo taasisi inayopambana na kuzuia ruswha, ambspo kwa kiasi kikubwa inazidi kupambana kadri iwezevyo ili kuendelea na udhibiti kwa wale wote wanaofanya vitendo hivyo vibaya na kuondoa ubadhilifu katika jamii yetu na kulijenga taifa moja lenye nguvu

4. Uvunjifu wa haki za kibinadamu, ambapo haki za binadamu zimekuwa zikivunjwa kila kukicha watu wanadhalilishwa, wanauawa na kufanyiwa mambo ya kikatili ambapo jamii yetu inakataza kwa nguvu pia hili linarudisha maendeleo nyuma

Pia ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara hata raia kuwa ni kikwazo cha kimaendeleo katika nchi yetu kwa kukwepa kulipa kodi ambapo kodi hiyohiyo inategemewa na serikali ili kuendeleza miradi ya kimaendeleo na kukuza uchumi wa taifa

Na mengineyo ni kama wizi, ujambazi na pia migogoro ya ardhi na uvunjifu wa haki za watoto na wanawake.

Hivyo ni jukumu letu kama jamii kuhakikisha Vikwazo hivi viondolewe ili kuzidi kuimarisha umoja, amani na maendeleo ya nchi yetu

Asante
 
Upvote 0
Back
Top Bottom