Hammy Js
JF-Expert Member
- Sep 20, 2017
- 3,054
- 3,263
Habari wana jf
Nimeona ni vyema kuanzisha thread hii ili watu waweze ku-share fursa mbali mbali za kujiingizia kipato walizowahi kuzifanya ama wanazozifanya kwa sasa au hata zile wanazozifikiria au kuziona mahali fulani zikifanyika.
Lengo hasa ni kupeana mbinu na ujuzi kuhusiana na fursa mbali mbali ambapo itasaidia kuwapa mwanga wale waliokuwa wakizifuatilia fursa hizo.
Binafsi, ninafikiria kununua incubator kwa ajili ya kutotoleshea mayai ya kuku ambapo baadae (baada ya utotoleshaji) nitakuwa nikiuza vifaranga.
Nimelenga kununua incubator itakayokuwa inatumia mafuta ya taa (nishati inayopatikana muda wowote) yenye uwezo wa kubeba trey kumi za mayai na zaidi (kama trey 12 hivi). Machine hii inatumia mafuta kuanzia Lita 7 mpaka 10 kulingana na hali ya hewa na bei yake haizidi sh.350,000/=
Bei ya trey moja ya mayai (kuroiler) huwa inaanzia sh. 13,000/= mpaka sh 15,000/=
Bei ya kifaranga (kuroiler) cha siku moja huwa inaanzia sh 1500 mpaka 2000/= kutegemeana na eneo pamoja na uhitaji na huwa inaongezeka kulingana na umri wa kifaranga.
Bado nipo kwenye hatua za ufatiliaji zaidi kwani ndio nataka kuianza (sikuwahi kuifanya kabla). Malengo yangu juu ya biashara hii ni kuja kuwa na poultry farm kubwa hapo baadae, hivyo ninaanza na mtaji mdogo kwa kujifunza ili nijue changamoto zake.
*******KARIBUNI******