Tushirikishane: Kipi hutasahau kwa mwaka huu

Tushirikishane: Kipi hutasahau kwa mwaka huu

Medecin

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
8,221
Reaction score
22,496
Maisha Ni mapito Na mapitio Kuna mengi yanatokea ambayo hubaki kama kumbukumbu kwa muda mrefu vichwani mwetu. Mwaka unaelekea ukingoni.

Tusimulie jambo lolote ambalo hautalisahau lililokutokea iwe mafanikio au mateso kwenye mapenzi,kazi,biashara au mihangaiko mingine ya kimaisha.

[HASHTAG]#Binafsi[/HASHTAG] nimepitia mambo mengi lakini kubwa la mafanikio ni kuwa nimeweza kufungua biashara kadhaa ambazo bado ziko stable pia natarajia kupata mtoto mwakani januari. Lakini kwa upande wa matatizo mojawapo ambalo sitalishau ni kupelekwa polisi na kulazwa mahabusu kutokana na kupigana na trafiki baada ya kunibambikia kosa. Hayo ndiyo ambayo sitayasahau kwa mwaka huu......

Pia kwa humu Jamiiforum nimefanikiwa kuanzisha Uzi pendwa wa Kupeana Likes ambao umekuwa namba moja kwa kuzipiku nyuzi nyingi za zamani.

[HASHTAG]#Tueleze[/HASHTAG] na wewe kipi hutasahau...............!
 
Siwezi kusahau fursa nyingi sana alizotushirisha boss ONTARIO bila roho mbaya yoyote May GOD bless him katika mambo yake ya kukuza uchumi wa Taifa.japo mi sijafanikiwa hata moja kutokana na financial problem[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
kweli kabisa ONTARIO anastahili pongezi sana. Amekuwa chachu ya mafanikio ya watu wengi humu kupitia forex Na mada zake nyingi za ujasiriamali.
 
Sitasahau nilivyoitwa mzushi na kupelekwa jela kisa nimeonyesha majengo yenye nyufa.

NB. Namjibia Kumbusho
haaa haaa haaa mzushi kwa kuwaonyesha expansion joints
 
Mimi sitasahau kile kipigo nilichokipata pale ukonga Mombasa baada ya kushuka kwenye daladala mida ya saa sita usiku hadi mkono uliteguka hawa police hawa nawachukia ile mbaya nikiona police analiwa na simba nitamsaidia simba police namuacha afe
 
Mwaka huu nimefanikiwa kutunikiwa shahada yangu ya kwanza ya food science and technology. Namshukuru sana Mwenyezi mungu kwa hilo na natamani sana kuendelea na elimu ya juu zaidi.
hongera Sana mkuu
 
Mimi sitasahau kile kipigo nilichokipata pale ukonga Mombasa baada ya kushuka kwenye daladala mida ya saa sita usiku hadi mkono uliteguka hawa police hawa nawachukia ile mbaya nikiona police analiwa na simba nitamsaidia simba police namuacha afe
au ukimkuta police anataka kumezwa Na chatu unamtafutia chatu mlenda Ili ammeze haraka. Nina marafiki polisi ila siwaaminigi kabisa
 
Sintosahau kuokota buku 10 sokoni kwa hali hii vyuma vilivyokaza hadi unalisahau jina lako
 
Kwa mwaka huu..
June 6 sitasahau nilipokuta geto wamenioaha Laptop Toshiba, SamsungS6, Begi la mgongoni, Pasi na Heater.

19 september natoka Zenji nakuja Dar tukanusurika kuzama ajili ya wimni.
 
Back
Top Bottom