mwaka huu siwezi kusahau nilivyopambana kutuma maombi ya ajira utumishi. Nilikuwa natumia zaidi ya laki mbili kila nilipoitwa kutoka mkoani kuja Dar kufanya interview. Mwishoni nlikata tamaa, nikasema sirudi tena Dar kwa ajili hiyo ya interview na maombi utumishi situmi tena. Nashukuru Mungu biashara niliyo amua kuifanya inaenda poa, mwezi wa 9 mwishoni nilifanikiwa kwenda Nairobi kwa mara ya kwanza. Nilichukua mzigo nikaleta bongo vizuri tu. 2018 naplan niagize mzigo kutoka Dubai au China. Mungu nisimamie nitimize ndoto zangu, amina!