Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Watu wengi wana mawazo mazuri ya biashara, lakini changamoto ni mitaji; wapo wengine wana wazo ambalo ukilipima unaona kweli ukiwekeza kuna faida mbeleni. Na wapo wenye mitaji lakini hawana mawazo ya biashara ila wanatamani wafanye biashara. Wazo likiwa ni laki-ujuzi itakuwa ni bora zaidi,kwa sababu litachochea kwenye utengenezaji wa bidhaa na si uchuuzi:-
Mfano:-
Mfano:-
- Labda wewe ni mtaalamu wa meno huna kazi ila una wazo na uko tayari mtu afungue clinic yake akuajiri.
- Labda wewe unaujuzi wa kuvundika vyakula na uko tayari kuajiriwa iwapo mtu atawekeza kwenye wazo lako
- Labda wewe ni fundi nguo/viatu n.k una wazo na uko tayari kuajiriwa na yule atakayewekeza kwenye wazo lako
- Labda wewe ni fundi magari unawazo ambalo mtu akiwekeza utakuwa uko tayari akuajiri n.k
- A. Tsh. 1000 - 99,000
- B. Tsh. 100,000 - 500,000
- C. Tsh. 510,000- 999,000
- D. Tsh. 1,000,000- 5,000,000
- E. Tsh. 5,100,000-10,000,000
- F. Tsh. 10,000,000+