Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,941
- 2,044
Asubuhi moja ya Oktoba 2021, Kijana wa umri wa miaka 18 aitwaye Michael, mkazi wa Tabora, alikutwa chumbani kwake akiwa kajinyonga kwa kutumia shuka. Kwanini ajinyonge? Jibu lilikuwa pembeni ya mwili wake. Alikuwa ameacha ujumbe kwenye karatasi. Ujumbe mfupi tu. Haukuwa unazidi hata maneno kumi. Ujumbe ulikuwa ni maneno tisa; “Mama naomba unisamehe ni maisha tu yamenifanya nijiue mnizike.”
Inasikitisha!
Kwenye tukio lingine, miaka kadhaa iliyopita nikiwa napitia nyuzi humu JF, kuna bwana mmoja alitoa malalamiko kwamba baada ya mdogo wake kufeli mtihani wa kidato cha nne alianza kuonesha dalili za kuchanganyikiwa - Alikuwa anaongea maneno yasiyoeleweka na kufanya vitendo vya ajabu ambavyo mtu wa kawaida hawezi kufanya – Jambo moja aliloonyesha ilikuwa ni kuvutiwa na wanawake kupita kiasi na hofu ya mleta uzi ilikuwa ni kwamba siku moja angeweza kuwabaka dada zake na wanawake waliopo hapo nyumbani au hata kuwadhuru. Nilipopitia maoni nilisikitika. “Karogwa” ndiyo yalikuwa majibu ya watu! Ila ukweli ni kwamba “mdogo wa mleta uzi ule” hakuwa amerogwa. Ilikuwa ni Skizofrenia. Au kwa lugha rahisi moja ya magonjwa mengi ya afya ya akili!
Michael na “mdogo wa mleta uzi ule” ni mfano wa watu wengi ambao wanapitia changamoto ya afya ya akili.
Utauliza afya ya akili ni nini?Afya ya binadamu inamaanisha afya ya kimwili, kiakili na kisaikolojia kwa ujumla. Mazingira anayokaa mtu yanaathiri sana afya yake kwa nafasi kubwa. Mara nyingi watu hulalamika kuhusu afya ya kimwili tu na wanasahau afya ya akili na kisaikolojia. Ni rahisi kutambua mabadiliko ya mwili kwa dalili kama mafua, joto la mwili, maumivu ya kichwa au UVIKO-19. Lakini si watu wengi sana wanajua kufuatilia afya zao za akili.
Hivyo kukosa elimu ya afya ya akili na imani za kishirikina zinawaacha watu wengi kwenye mateso na maumivu ya ndani kwa ndani. Afya ya akili inahusisha kuanzia namna unavyofikiria, unavyohisi, pamoja na matendo yako. Hii inamaanisha maisha yako yanaathiriwa na afya ya akili kuanzia kijamii, kikazi na maisha binafsi. Afya ya akili ikiathirika inakuwa ni hatari kubwa sana kwa mhusika!
Baadhi ya sababu za watu kupatwa na tatizo la afya ya akili.
Mazingira: Kuishi kwenye mazingira magumu inaweza kusababisha mtu apate tatizo la afya ya akili. Mazingira kama umaskini au kuwa na familia ambayo inakunyanyapaa na kukudharau.
Malezi na mikasa aliyopitia mhusika kipindi cha utoto: Hata kama ukiwa haupo kwenyemazingira magumu, mikasa uliyopitia utotoni inaweza kukusababishia tatizo la afya ya akili.
Matukio ya kuhuzunisha: Matukio kama kupoteza umpendaye, au kutokufanikiwa mipango yako ni moja ya sababu za kupata tatizo la afya ya akili.
Matumizi ya pombe na madawa ya kulevya: Hii ni sababu ya vijana wengi kujikuta tayari wana matatizo ya afya ya akili, na mara nyingi husababisha ugumu kupona.
Watu wengi wenye matatizo ya afya ya akili hawajui namna nzuri ya kushughulikia matatizo yao ya afya ya akili, hivyo wanatumia njia ambazo zinaongeza hatari zaidi. Matokeo yake wanaishia kwenye matumizi ya dawa za kulevya, pombe au kujiua wakidhani hizi ni njia sahihi. Ila ukweli ni kinyume chake.
Ingawa kila mtu ana haki ya afya bora bila kujali hali yake ya kiuchumi na kijamii, ni watu wachache sana wanaoweza kupata elimu ya afya ya akili. Hivyo kuna haja ya serikali na taasisi zisizo za kiserikali kuwekeza kwenye ukanda huu. Ziandaliwe semina, makala, vitabu na filamu ili jamii itambue umuhimu wa afya ya akili.
Kuwa na afya bora ndiyo njia pekee ya kuishi maisha yenye maana na yanayotakiwa. Kwa ulimwengu wa sasa ambao umejaa uongo wa mitandaoni na changamoto nyingi za kimaisha inakuwa ni rahisi sana afya za akili kuathirika haswa rika la vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa lolote lile. Tena kwa jamii hii ambayo inachukulia mambo kwa kawaida sana. Hatari inakuwa kubwa zaidi.
Ni wakati sote tubadili imani zetu kuhusu suala la afya. Tusiishie kuzingatia afya ya mwili tu. Inapaswa kuizingatia afya ya akili na kisaikolojia pia kama tunataka kuishi vyema. Hata hivyo kuna baadhi ya vitu vichache ambavyo ukivizingatia unakuwa na nafasi kubwa ya kuwa na afya njema kwa ujumla – Yaani kimwili, kiakili na kisaikolojia.
Fanya mazoezi mara kwa mara: Mazoezi ni sehemu muhimu sana ya afya ya binadamu na kuyafanya au kutoyafanya kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa hali ya afya ya mtu. Hivyo ni jambo muhimu sana na inashauriwa na madaktari.
Kula vyakula sahihi: Kutumia chakula sahihi itakusaidia sana. Jaribu kuacha kutumia vyakula vya kufungasha. Vyakula vya mafuta na uongeze tabia ya kula matunda na mbogamboga. Pia kula chakula bora itakusaidia sana kuwa na afya imara.
Kunywa maji ya kutosha: Sio kila mtu anafahamu umuhimu wa kunywa maji mengi. Moja ya faida ya maji itakusaidia kuweka uzito wako sawa. Pia maji yanasaidia sana mwili kukamilisha shughuli zake. Usitafute sababu ya kuacha kunywa maji. Hakikisha unatembea na kopo la maji kila unapoenda.
Pumzisha mwili: Njia nyingine nzuri ya kuilinda afya yako ni pamoja na kulala usingizi wa kutosha. Jitahidi kulala mapema na kuamka mapema. Hakika utaona mabadiliko kwenye afya yako kama utajiwekea ratiba nzuri ya kupumzika.
Fanya vipimo mara kwa mara: Jitahidi kupima afya yako kila wakati. Wengi wetu huwa tunasubiria mpaka hali iwe mbaya ndipo tupime, ila hili ni kosa. Kupima mara kwa mara kutakusaidia kujua na kuelewa afya yako mapema kabla haujazidiwa na magonjwa. Kinga ni bora kuliko tiba!
Punguza mawazo: Mawazo ni ugonjwa mbaya sana!. Mawazo husababisha kula sana, kulala kupita kawaida na sonona ambayo itapelekea matatizo makubwa kwenye afya yako kiujumla na ndiyo maana baadhi wanaenda kujiua. Lakini ukishirikisha watu kwenye matatizo itapunguza uwezekano wa wewe kuathirika na afya yako.
HITIMISHO: Serikali, taasisi zisizo za kiserikali na watu binafsi wafanye jitihada za kutoa elimu kwa jamii, haswa makundi yanayoathirika, kuhusu elimu ya afya ya akili. Hii itapunguza hatari zinazowakumba wahusika kama Michael na wengine wengi.

Upvote
10