Kikwava
JF-Expert Member
- Sep 6, 2015
- 1,741
- 1,068
UTANGULIZI
Kumekuwa na desturi ya kuchagua wabunge wetu kwa mazoea, yani hakuna upimaji wowote unao ainishwa kwamba mbunge kabla ya kugombea awe amefanya hiki na kile au baada ya miaka 5 awe amefanya na kukamilisha Jambo fulani na endapo akishindwa kukamilisha Jambo hilo iwekwe wazi kwamba hata ruhusiwa kugombea tena, Sasa nini kifanyike? Yafutayo yakitekelezwa kwa ufasaha yataongeza Uwajibikaji wa wabunge wetu;
1. Kamati za wajumbe katika ngazi za vijiji kata na tarafa,
Hizi kamati zikae mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, ziainishe yapi wanapendekeza yafanywe na mbunge wao pale tu atakapo Anza kazi Kama mbunge, kwamfano sehemu au Jimbo ambalo ni Mji, kazi ya mbunge iwe ni kuhakikisha anaupigania mji (Town council) kuwa manispaa kwa kuhakikisha anapigania uboreshaji wa miundombinu na kuutanua mji kupitia upimaji wa viwanja na kutoa ramani rasmi ambazo zitakuwa mwongozo wa wote watakao Jenga maeneo husika ili kuupendezesha mji.
2, Uundwe umoja wa wenyeviti wa mitaa/vijiji kwenye Jimbo,
ambao watatumia sehemu ya mapato ya mitaa/vijiji Kama posho na nauli ili waweze kukutana Mara mbili kila baada ya miaka mitano kwa lengo la kumfanyia tathimini mbunge wao, baada ya tathimin nakala ya repoti imfikie mbunge wao na katibu wa chama husika, repoti itamke wazi mapungufu na mafanikio ya mbunge husika na mwishoni kuwe Kuna maoni kwamba wanashauri aendelee au ampishe mtu mwingine kwenye uchaguzi ujao, hii itaongeza Sana Uwajibikaji kwa waheshimiwa wabunge.
2. Sifa za mbunge,
Kwasababu ngazi ya ubunge ni kubwa kwenye Taifa letu na jamii yetu, kuwe na vigezo vya mtu kugombea na kuwa mbunge, mbunge awe na sifa za pekee katika jamii, Kama ni Elimu basi iwe Elimu ambayo itamheshimisha na itaendana na masilahi ya ubunge. Mfano mbunge awe labda na PhD au mbunge awe na Utajiri wa kiasi fulani Cha fedha ndipo aruhusiwe kuchukua fomu ya ubunge. Hii pia itamuongezea mbunge ari ya kuwatumikia wananchi na kuongeza Uwajibikaji katika kazi zake za ubunge, kwamba mbunge akiwa tajiri basi atakuwa ana uwezo wa kuwasaidia wananchi wake bila kusubiri msaada kutoka serikali kuu, akiwa msomi basi ataweza kung'amua na kuyamaliza matatizo ya wananchi wake kwa kutafuta njia mbudala wa kutatua matatizo,. Kwa mfano eneo husika halina daraja basi mbunge ataweza kuandika andiko (proposal) kwa wadhanini na wakaweza kumjengea daraja sehemi husika.
3. Wajibu wa chama Cha siasa kwa mbunge.
Chama Cha siasa ndicho kinachotoa mbunge ili aingie kwenye kinyang'anyiro kwahiyo chama Cha siasa kina nafasi kubwa ya kuhakikisha kinampata mtu ambaye hana makandomakando ya rushwa na historia mbaya ya utendaji kazi. Nini kifanyike na chama Cha siasa husika? Yafuatayo Napendekeza yafanyike ili kumpata mgombea sahihi wa Jimbo husika
3.1. Kuwe na ada kubwa ya fomu.
Chama husika kitoze kiasi kikubwa cha fedha ya kuchukulia fomu, kwamfano, fomu inunuliwe kwa Tsh. 10,000,000/= hii itatumika pia kwa kiasi fulani kupima uwezo wa kifedha wa mgombea na chama husika, pia chama kifatilie kijue kazi rasmi ya mgombea wake iliyomfanya awe na kiasi hicho Cha fedha ili isije ikawa kazipata kwa njia ya rushwa.
3.2 Mgombea aonyeshe Kazi za maendeleo ambazo ameshazifanya kwenye Jimbo husika,
kwamfano amejitolea kujenga madarasa mangapi, ametoa mikopo kwa kina mama na vijana kwa kiasi gani, ameshiriki vipi kwenye shughuli za kawaida kwenye Jimbo husika, hii itaondoa tatizo la kupata wabunge wababaishaji ambao wanategemea kupita kwenye Kura za maoni kwa kuwanufaisha watu wachache (wajumbe) na kuacha watu waliowengi bila msaada wowote.
3.3. Mgombea awe ni yule anayekubalika na wajumbe wengi kwamba siyo mgeni kwa jamii husika kwa maana kwamba amekuwa akijitabaisha hata kwenye vyombo vya habari kwa kutoa mapendekezo ya kimaendeleo ya nini kifanyike ili kuhamasisha maendeleo kwenye Jimbo husika, siyo mtu anaoneka siku ya kuchukua fomu tu hii haileti afya kwa jamii kwasabu anakuwa mgeni kwa wananchi walio wengi.
4. Ukomo wa mbunge iwe ni miaka 10.
Baada ya miaka 5 mbunge afanyiwe tathimin na umoja wa wenyeviti wa mtaa wa Jimbo Kama nilivyopendekeza kwenye kipengere namba 2. hawa wenyeviti wa mitaa na vijiji watatoa mapendekezo Yao ya mbunge aliyekuwepo aendelee au akabidhi kwa mtu mwingine Kama ataendelea basi atatumikia kwa muda wa miaka 5 mingine na hataruhusiwa kugombea tena.
Imetolewa na Mimi Kikwava (MA)
Naomba Kura yako
INSHALLAH 🙏🏼

Upvote
4